Sunday, 5 February 2017

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI RUFAA YA TRUMP.



Mahakama ya rufaa nchini Mareni imekataa ombi kutoka kwa idara ya haki nchini humo la kutaka kurejeshwa amri ya Trump ya kupiga marufuku wasafiri kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

SHULE IMEFUNGA CCTV CAMERA KUDHIBITI NIDHAMU YA WANAFUNZI.

Tafakari haya, ndani ya shule ya upili, kuna kamera zilizotundikwa katika kila pembe ya shule ili kuboresha nidhamu. Mwanafunzi anapokiuka sheria na kanuni za shule basi hana lake kwani ushahidi utanaswa kwenye kamera. Ndivyo mambo yalivyo katika shule ya upili ya wavulana ya Karima katika eneo la Othaya. Isitoshe, kando na kamera hizo, kuna mashine zinazotambua alama za vidole za mwanafunzi na kutuma ujumbe mfupi kwa mzazi iwapo mwanafunzi huyo anaingia au kutoka shuleni.

Lakini jambo kubwa la kujiuliza ni je hii ni njia sahihi ya kudhibiti nidhamu ili kama inafaa basi shule nyingine pia ziige mfano huu kwenye maeneo yetu? 

Unaweza kuandika maoni yako kwenye blog au kwenye tweeter na facebook.