WATU WALIOKATALIWA KUISHI NCHI KAVU.
Wabajui huishi na familia zao kwenye vibanda vyao vya miti vilivyojengwa baharini kwani wamezuiwa kuishi nchi kavu na pia pia wakikaa sana nchi kavu wanajihisi kuumwa. Dunia ina mambo mengi sana, mengine yanastaajabisha, mengine kuudhi na mengine kufurahisha. Ila hili sijui linaleta picha gani. Bahari ni makazi ya karibu nusu ya viumbe hai waishio duniani ila sisi binadamu sio mojawapo ya viumbe hivyo kwani hatuwezi kukaa ndani ya maji ya chumvi kwa muda mrefu, hatuwezi kuzama na kukaa kwenye kina cha bahari kwa muda mrefu lakini kinyume na haya yote kuna baadhi ya binadamu karibia maisha yao yote ni baharini! Wamejenga "vijumba/vibanda" vyao vya miti huko na asilimia zaidi ya 90 wanaishi huko na sio nchi kavu! Naam, ni watu jamii ya