Tuesday, 26 July 2016

MATAIFA YENYE WATU WAREFU ZAIDI DUNIANI.

Utafiti mpya umeonesha kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake, wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.
Kimo cha wastani kwa wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimeta 183), na kimo cha wastani kwa wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimeta 170).

KOFFI OLOMIDE ATAMATWA DR CONGO


Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Mwandishi wa BBC Poly Muzalia anasema mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la afisi ya mwendesha mashtaka.

JINA LA CHRISTIANO RONALDO KUTAWALA VITU VYA MJI WAKE WA NYUMBANI.


Uwanja wa ndege wa mji wa nyumbani kwa mwanasoka bora mara tatu wa dunia kupewa jina lake ili kuuenzi mchango wake katika soka la nchi hio.

MPASUKO NA SINTOFAHAMU NDANI YA CHAMA CHA DEMOCRAT


Kiongozi wa Chama cha Democratic nchini Marekani amesema atajiuzulu baada ya barua pepe zilizofichuliwa na kuchapishwa na mtandao wa WikiLeaks kudokeza huenda maafisa wakuu wa chama walijaribu kuvuruga kampeni ya Bernie Sanders.

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATOA LA MOYONI.

TAMKO MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUKEMEA UKIUKWAJI WA HAKI ZA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NA KUZUILIWA KWA MAWAKILI KUFANYA KAZI ZAO
UTANGULIZI

HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA KUU JUU YA KESI YA DAUDI MWANGOSI.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi Pacificius Cleophace Simoni kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Sunday, 24 July 2016

MOYES APATA KIBARUA SUNDERLAND

OFFICIAL: SUNDERLAND WAMTHIBITISHA MOYES KUA KOCHA MPYA.



Kocha wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester united na Real Sociedad ametangazwa rasmi kua kocha mkuu wa paka weusi (klabu ya soka ya Sunderland) kuchukua mikoba iliyoachwa na Sam Allardeyce ambaye analwenda kuifundisha timu ya taifa ya England (Simba watatu).

NDEGE INAYOWEZA KUPAA NA KUTUA MAJINI.


China imeunda ndege kubwa zaidi duniani ambayo ina uwezo wa kupaa au kutua kwenye maji au uwanja wa ndege.
Ikizinduliwa ndege hiyo ilishangiliwa na umati wa watu katika mkoa ulio kusini wa Guangdong.

MBARONI KWA KUTAKA KUIBA MWNGE WA OLYMPIC.

Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.

KOFFI OLOMIDE ATIMULIWA KENYA NA VISA YAKE KUFUTILIWA MBALI


Mwanamuziki maarufu wa asili ya Congo, Koffi Olomide, siku ya Jumamosi alifukuzwa kutoka Kenya na serikali ya nchi hiyo baada video iliyomuonyesha akimpiga teke mmoja wa wacheza densi wake kulaaniwa vikali, hususan na Wakenya mitandaoni.

WAVULANA WATINGA SKETI SHULENI.

Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.