Saturday, 6 May 2017

MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI. (2)

Muendelezo wa vitisho baina ya korea kaskazini na Marekani kwa mwezi wa nne 2017.

 Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC)

April
Korea kaskazini ilirusha kombora jingine kulenga bahari ya Japan na kitendo kilichozua hofu kubwa toka Japan.
Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.

Tuesday, 2 May 2017

MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (1)

DUNIA YA VICHWA VIWILI VISIVYOTOSHANA.

Meli ya kubeba ndege na makombora ya Marekani ikiwa njiani kuelekea eneo la bahari la korea kufuatia mvutano mkali baina ya Korea na Marekani.


Kuna wasiwasi wa dunia kutumbukia kwenye vita mbaya ya nyuklia kutokana na vitisho baina ya Marekani na Korea kaskazini. Kumekuwepo na vita za maneno na vitisho baina ya Washington na Pyongyang watishiana kupigana baada ya kipindi kirefu cha bila maelewano baina yao.