Friday, 27 October 2023

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA-3

 

HAMAS: KUTOKA KIKUNDI CHA KUTOA MISAADA MPAKA KIKUNDI CHA KISIASA NA KIJESHI.

                                 Jeshi la Israel 

Ili kuelewa imani na itikadi kali ya Hamas kabla hata kuundwa kwake tuone kidogo ikitikadi ya Waarabu juu ya taifa la Israel hasa kabla ya vita vya siku sita [5-11 June 1967]. Hizi ni kauli za kukupa picha HAMAS wanasimamia nini na Wanapigania nini.

Radio Cairo ilitangaza kua "[Watu] Waarabu wamedhamiria kikamilifu kuifuta Israel katika ramani na kirejesha heshima ya watu wa Palestina". May 25, 1967.

May 28, 1967 rais wa Misri Gamal Abdel Nasser anasema  "Hatutakubali uwezekano wowote ule wa Israel na Palestina kuwepo pamoja".

31 May 1967 rais wa Iraq Abdel Rahman Aref anasema "Uwepo wa Israel ni dosari ambayo ni lazima irekebishwe".

Utaona msimamo mkali wa Waarabu dhidi ya Israel kwa hio salama ya Israel ilikua ni kupitia kujua namna gani atakua wa kwanza kujilinda dhidi ya maadui zake ambao wote wanatangaza kumuangamiza.

Sasa kwanini HAMAS ilianzishwa turudi 29 August 1967 kule Khartoum Sudan kulikaliwa mkutano wa Shirikisho la nchi za Kiarabu (Arab League) iliokua na makao makuu pale Cairo, Misri. Katika kilele cha mkutano huo Arab League ilikuja na azimio la HAKUNA/HAPANA TATU (THREE NOES) ikiwa ni No peace with Israel, No recognition of Israel na No negotiation with Israel [ Hakuna amani na Israel, Hakuna kuitambua Israel na Hakuna majadiliano na Israel]. Na hili linaanzia katika imani ya Waarabu hata kabla ya vita mfano tizama msimamo wa Misri na Iraq kabla ya June 5, 1967.

:::::::::::::***

MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA SEHEMU YA 2

KUUNDWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA "KUTOWEKA" KWA PALESTINA.  

Ramani ya mgawanyo wa maeneo kati ya Israel na Palestina [1948]
Jinsi ambavyo Israel na Palestina zilivyo kwa sasa

Katika makala hii tutatazama kushamiri kwa mzozo kati ya Waisraeli na Palestina kuanzia 1948 hadi sasa. Hebu tuanze na haya maneno na badae itakusaidia kuelewa vyema. 

Nakba ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha "Janga Kuu" yaani "Catastrophe". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kuanzia 1998 siku hii imekua ikisherekewa kama kumbukizi kwa Wapalestina. 

Ha'atzmaut ni neno la Kiebrania likimaanisha "Uhuru". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kwa hio tukio lile lile upande mmoja unatambua kua ni Janga kuu na upande mwingine ni Uhuru. Utata unàanza kwamba vita rasmi ya Palestina na Israel ilianza saa ileile ambapo Irael ilijitangaza kwamba ni taifa huru ndani ya taifa huru la Palestina!

Tuesday, 24 October 2023

ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?


Picha kwa hisani ya mtandao


ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI? 

"Vita havina macho". Ni msemo tu katika jamii nyingi ukiwa na onyo la kutokushadadia vita. 

Tarehe 7 Oktoba 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi kwa saa za Israel, kulitokea shambulio la kushtukiza kutoka kikundi cha HAMAS ambacho kwa tafsiri ya Marekani na washirika wake ni kikundi cha kigaidi. 

Tukio hilo lilidhihirisha udhaifu katika idara ya ujasusi ya Israel kwa maana ya Mosad pamoja na Shin Bet. Kikubwa zaidi ni kile kilichokuja kuwa ni kisasi cha Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza.

Itoshe kusema mitaa mingi ya Gaza City imekua kama mji wa Kale uliokumbwa na kisa cha kutisha mno. Imekua kama "Ghost City". 

Tangu hapo kumekuwa na maoni tofauti juu ya nani yuko sahihi katika hili. Ukweli ni kwamba katika wakati huu ni swali baya ila kikubwa ni nani atasalia? Achilia mbali kua sahihi.