UTAWALA WA SHERIA vs WATAWALA WA SHERIA. Hiki kichwa cha habari niliona kikiwa kwenye lugha ya kingereza. Ni kitabu kilichoandikwa na Prof. Issah Shivji akielezea maisha ya Jaji mkuu mstaafu Barnabas Albert Sammata. Nilipenda kukisoma kitabu hiki lakini sikufanikiwa. Ila nilifanikiwa kupata dhima ya juu ya kitabu. Lakini nilipenda maneno machache tu ya jaji samata ambayo nami ntayatumia hapa. Aliwahi kusema "Let everyone in our society give justice a chance to prevail".(Hebu tufanye kila mmoja wetu katika jamii aipe haki nafasi ya kukua"[tafsri sio rasmi]). Katika taifa lolote lile litakalokua linajiita ni taifa la kidemokrasia basi halina budi kuruhusu ustawi wa haki. Na haki itakuepo pale tu ambapo watu waliopewa dhamana ya kuisimamia wanakua na maadili. Amini usiamini ila kuna kazi hazihitaji saana maadili kama zingine. Uongozi ni kazi ambayo huwezi kuifanya kama huna maadili. Wanasaikolojia wanaamini ili kuweza kumjua mtu alivyo ni lazma tumjue kupitia tabia. ...