Saturday, 13 August 2016

RAISI MAGUFULI AMKUBALI MRISHO MPOTO


Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’.

MESI AKUBALI KURUDI TIMU YA TAIFA.


Nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Mesi ameamua kubadili uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu yake ya Argentina kufuatia matokeo mabovu ya timu yake kwenye fainali za michuano mikubwa. Mesi alifikia uamuzi huo kufuatia mazungumzo kati yake na kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza.

Thursday, 11 August 2016

HAKUNA "UBINAMU" NCHINI KENYA WANAKULAGA!

Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha uhusiano wa kimapenzi baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.

Wednesday, 10 August 2016

SIFA 5 ZINAZOKUONESHA KUA WEWE NI "SMART" KULIKO WENZAKO.

KAMA UNA VITU HIVI JUA WEWE UKO SMART KULIKO WENGINE.

Wanasayansi wamegundua vitu vitano vinavyoonesha kua wewe ni smart kuliko wengine.

1. Mtu anaetumia mkono wa kushoto(Left handed).
Ni zawadi ya ubunifu ulopewa tangu kipindi unazaliwa. Watu wanaotumia mkono wa kushoto wana maamuzi ya haraka kuliko wale wa kawaida(mkono wa kulia).

2. Mcheshi(sense of humor)
Kuna utafiti ulifanywa karne ya kumi na saba na ulionesha kua wachekeshaji wa IQ kubwa kuliko wengine.

3. Mzaliwa wa kwanza
Zamani ilikua mzaliwa wa kwanza anapewa urithi mara mbili ya wengine kwa kutambua thamani yake. Hata sasa wazaliwa wa kwanza wanaheshimika kwani wao ndio kioo cha ndugu zake wanaomfuata.

4. Kuchelewa kuamka
Wanasayansi wamegundua kua kua wale wote wanaochelewa kuamka ni bora kuliko wale wanaodamka asubuhi na mapema.

5. Introvert (Mndani)
Huyu ni mtu anaetegemea sana uwezo au vyanzo vya ndani kwaajili ya maendeleo yake. Zaidi 60% ya watoto wenye vipaji ni introvert. Wanatumia walivyo navyo ndani kuliko vilivyo nje.

Kwa sifa hizi je wewe ni smart kuliko wengine????

MASOMO YA SAYANSI NI LAZIMA KWA WANAFUNZI WOTE.







Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako.

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

HATARI TANO USIZOZIJUA KUHUSU SIMU YAKO.

MADHARA YA SIMU AMBAYO HUJAWAHI KUAMBIWA.


Kwa miaka mingi sasa kumekua na mijadala mikubwa kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya simu. Matumizi ya simu yamekua yakiongezeka kila kukicha. Sasa watu wanatuma ujumbe wa maneno, sauti,video, kuchati kwenye mitandao ya kijamii, kutazama video mtandaoni, kutumiana picha, kuperuzi, kusoma vitabu, majarida n.k kupiga picha za selfie n.k yote haya ni matumizi ya simu lakini swali kubwa linabaki "Je ni kweli matumizi ya simu hayana athari zozote kiafya?".

Sunday, 7 August 2016

TAARIFA RASMI YA MAN UNITED JUU YÀ POGBA












Ni taarifa iliyotolewa na manchester united kupitia tofuti yao. 

Headlines za kiungo wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea klabu ya Juventus ya Italia Paul Pogba kuhusishwa kujiunga na Man United, zinaelekea kumalizika kwa kiungo huyo kurudi Man United toka aondoke mwaka 2012.