WAAFRIKA WAUNGANA NA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA NCHI GHANA. UMAJUMUI WA AFRIKA UNAPATA NGUVU MPYA?
Moja kati ya bango likiwa na ujumbe kua "HATUDAIWI, HATUTOLIPA" Bara la Afrika ni moja ila ikiwa Waafrika ni wamoja ni swali pana sana na inaweza kua vigumu kufikia hitimisho la pamoja. Wakati wa Karne ya dhahabu kwa nchi za kiafrika naweza kusema ilikua ni kipindi cha miaka ya 1960s. Hapa tulishuhudia miito mbalimbali ya Waafrika kuungana na kua wamoja au kitu kimoja na mwaka 1963 viongozi wa nchi huru za Afrika walifanikiwa kuunda Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) lakini baadae mwaka 2002 Umoja wa Afrika (AU) ulianza rasmi baada ya Sirte declaration kule Linya mwaka 1999. Lengo lilikua ni kuwaleta Waafrika pamoja na kupigania haki na usawa katika nyanja za kimataifa. Kupitia mikutano na makongamano mbalimbali imekua dhahiri kua Afrika ina hitaji ukombozi mpya kwani sasa inaelekea kulekule tuliko toka kwenye miaka ya 1980s ambapo madeni ya nje yalizidhoofisha nchi za kiafrika na kufikia hatua ya kufilisika ndipo taasisi za kifedha za kimataifa na nchi wakopesha...