Tuesday, 18 April 2017

HISTORIA YA UHASAMA KATI YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI.




Rais wa marekani (kushoto) na rais wa korea kaskazini(kulia).


UJUE KWA UNDANI UHASAMA WA MAREKANI NA KOREA KASKAZINI. 

Siku za hivi karibuni kumeibuka mvutano mkali na vitisho baina ya mataifa hasimu kihistoria moja kutoka rasi ya korea na jingine kutoka amerika ya kaskazini. Mvutano huu umeongeza hofu ya kutokea kwa vita ya tatu ya dunia na imechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kila mahali. Lakini wengi hatufahamu hasa kwanini mataifa haya yamekua hasimu kwa kipindi kirefu na labda ndio uhasama mkali zaidi duniani. Maelezo haya yatakusaidia kuelewa kwa undani uhasama huu.