Saturday, 23 July 2016

KIJANA MMOJA AUWA KWA KUPIGWA NA MWEKEZAJI.



















Kijana mmoja aliyejukikana kwa jina moja (Elisha) mkazi wa Kabindi Mkoani Geita amefariki Dunia baada ya kupigwa na mchina kwa jina "Mr. Swii" kwa madai ya kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara. Taarifa zinadai waliopigwa wengine wawili wako hospitali kwa matibabu zaidi.

WALINZI ZAIDI YA 300 WA KIKOSI CHA KUMLINDA RAISI KUKAMATWA UTURUKI.

Uturuki imetoa warrant wa kukamatwa kwa zaidi ya walinzi 300 wa kikosi cha kumlinda raisi kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli tarehe 15 July 2016.
Inasemekana tayari walinzi 283 tayari wameshakamatwa na operesheni hio ingali bado inaendelea, liliripoti shirika la habari la Xinhua.

MLEMAVU APANDIKIZWA MIKONO YA MTU MWINGINE.

Uingereza imefanikiwa kufanya upasuaji na kumpandikiza mgonjwa mikono ya mtu mwingine.
Oparesheni hiyo imefanyika katika hospitali kuu ya Leeds ambako mgonjwa mwenyewe amesema amefurahia kurudishiwa viungo hivyo muhimu mwilini.

Friday, 22 July 2016

ULIIKOSA HII YA KOFFI OLAMIDE AKIMPIGA TEKE DENSA WAKE?

Msanii Koffi Olamide amenaswa na kamera akimpiga teke densa wake wakati wanawasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini kenya.

MAGARI YA UMEME YAANZA KUUZWA KENYA.


Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.

VYUO VILIVYOFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/17.

JE, TUNAWEZA KUEPUKA MALARIA KWA KUFUGA KUKU? SOMA UTAFITI HU.

Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,, Fuga kuku !
Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.

MAALIM SEIF KUTINGA MAHAKAMA YA ICC


Wakati polisi wakisema wanasubiri jalada la Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad litoke kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) ili wamfikishe mahakamani kwa uchochezi, leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali.

Wednesday, 20 July 2016

HATMA YA WANAFUNZI WALIOFULUZWA DODOMA

Kati ya wanafunzi elfu saba (7802) waliokuwa wamejiunga na chuo kikuu cha Dodoma Tanzania ni wanafunzi 382 pekee wenye sifa zitakazowaruhusu kurejea chuoni humo.

WANAWAKE WAOMBA WATAFUTIWE WANAUME WA KUWAOA.

Zaidi ya wanawake waislamu 10,000 wameomba watafutiwe waume watakaowaoa.

Tuesday, 19 July 2016

MKE WA TRUMP KWENYE KASHFA YA WIZI WA MANENO/WAZO.

Wizi wa maandishi wautia kiwingu mkutano wa Republikan
Donald Trump anakabiliwa na kashfa ya wizi wa maandishi au mawazo iliochafuwa hotuba ya mke wake Melanie katika mkutano mkuu wa chama cha Repuplican ambao ufunguzi wake umekumbwa na vurugu za wanachama wa kawaida.

MVUTANO WAZUKA KWENYE SIKU YA KWANZA YA MKUTANO WA CHAMA CHA REPUBLICAN.

Ghasia zatokea kwenye siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa chama cha Republican hapo jana baada ya wakuu wa chama kuzuia juhudi za dakika za mwisho za kubadili kanuni za mkutano.
Hoja ya kutaka wajumbe wapewa nafasi ya kuamua nani wanampendelea kumpigia kura badala ya kumchagua mshindi wa uchaguzi wa awali iliwasiloishwa na kundi linalompinda Trump.

NANI KUA MWANASOKA BORA KWA MWAKA HUU?

Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.

TOP 10 YA SIMU KALI ZILIZO SOKONI MPAKA SASA

Kila mtu anapenda kutumia kilicho bora zaidi. Sasa hapa nina orodha ya simu kali zilizoko sokoni mpka sasa 2016. Kama humiliki moja kati ya hizi....daah.

Monday, 18 July 2016

MWALIMU MKUU SEHEMU YA TATU(..3)

MWALIMU MKUU/ HEADMASTER 

SEHEMU YA TATU

Baadae nilimskia mwalimu mkuu kua anataka kupumzika...kila mwamafunzi alifurahi kwa kua aliamini atasoma kwenye shule aliyokua akiiota..

Endelea...

OMBI LA OBAMA KWA WAMAREKANI


Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA REPUBLICAN KUANZA LEO.














Jukwaa litakalokutumiwa na mgombea wa uraisi.

Maelfu ya wanachama na wajumbe wa chama cha Republican nchini Marekani wanakusanyika katika mji wa Cleveland, Ohio, katika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama hicho ambapo watakmteua rasmi bilionea Donald Trump kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Sunday, 17 July 2016

SABABU ZA UFARANSA KUANDAMWA NA MAGAIDI.

Sera za ndani na nje  za ufaransa zaigeuza muhanga wa mashambulizi. 
Baada ya mashambulizi mawili yaliyouwa watu 17 mjini Paris mwezi Januari 2015, gazeti la Dar al-Salaam linalomilikuwa na "Dola la Kiislamu" (IS) lilichapisha Mnara wa Eifell likiandika "Allah ilaani Ufaransa."

WAAFRIKA SASA KUA NA HATI MOJA YA KUSAFIRIA.


Je unamiliki cheti cha kusafiria cha taifa lako?
Hivi Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !
Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.

UFAFANUZI WA TCU JUU YA VIWANGO VYA UDAHILI.

Kufuatia tangazo lililotolewa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) wiki iliyopita kumekua na sintofahamu miongoni mwa wadau na wanafunzi juu ya sifa na vigezo vitakavyotumika kwenye udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Mapema wiki iliyopita TCU ilibanisha kua ili kujiunga na chuo lazima uwe na alama D ambazo ni pointi 4.