Posts

Showing posts with the label KIMATAIFA

BAADA YA MIAKA 113 KANISA LAHAMISHWA BILA KUVUNJWA.

Image
Kanisa la Lutheran la Kiruna huko Sweeden likiwa tayari kusafirishwa. Picha kwa hisani ya Forbes Katika hali ambayo sio ya kawaida kanisa moja la kihistoria huko nchini Sweeden limehamishwa kutoka sehemu mabo lilijengwa na kupelekwa sehemu nyingine baada ya miaka 113 la kuwepo katika eneo ambapo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1912. Kuhamishwa kwa kanisa hilo la Lutheran ni kutokana na kuwepo kwa uchimbaji wa madini ya chuma chini ya kanisa hilo na maeneo mengine ya jirani. Mpango wa kuhamisha kanisa hilo bila kubomoa umekua ukiendelea kwa takribani mwaka mmoja ambapo wataalam wamekiri kwamba haikua kazi rahisi. 

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

Image
AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? HATIMAYE AFRIKA IMEANZA KUZINDUKA. Ramani ya dunia  Tulipokua shuleni tulijifunza mengi juu ya Afrika lakini mengi ilikua ni upotoshaji wa kukusudia au kutokukusudia. Hilo linajidhihirisha pale unapotazama ramani ya dunia. Utaambiwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani nyuma ya Asia lakini ukitazama ramani utagundua Amerika ya Kaskazini inaonekana kuwa ni kubwa kuliko Afrika. Lakini je Afrika ina ukubwa gani? Na kwanini sasa Umoja wa Afrika unahitaji taasisi kuu ulimwenguni kote kutumia ramani mpya ya Afrika kulikoni?  Tunarejea takribani miaka 456 hivi nyuma kuanzia sasa. Tunakutana na mwaka 1569, na hapo tunakuja kukutana na mtu mmoja aliyepata kua ni mwanajiografia na mchora ramani kutoka Flanders (Kijiografia eneo hili liko Ubelgiji na kijamii na kiutamaduni limekaliwa na watu asili ya Wadachi). Mtu huyu alitwa Gerardus Mercator ambaye ndiye aliyechora ramani hii ya dunia ambayo katika karne ya 18 ilirasmishwa kutumika katika maswala ya usa...

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA

Image
 Volume 1 | Issue 1 2023/09/24 Meli ya kivita ya Marekani Picha za mtandao Historia ya Taifa la China . Tofauti na Marekani, taifa la China lina umri mrefu sana. Uchina ya kale (“Ancient China”) imekuepo tangu miaka 2000 Kabla ya Kristo/ Kabla ya kipindi cha sasa (2000BC/BCE). Wakati huo Uchina ilikua imegawanyika katika koo mbalimbali kama Zhang, Zhou, Quin, Han na nyinginezo. Ugunduzi wa kale wa risasi, dira, maandishi na uchapaji vilianzia huku. Historia yake ni ndefu mno, hatutoweza kuiandika yote.

MAAJABU YA JAPANI

Image
Photo credit: the crazy tourist.com Kuna mambo mengi hutokea duniani na katika jamii flani yakiwa na upekee kabisa kutoka upande au pande nyingne za dunia. Na Japan ni moja ya mataifa ambayo kwa kiasi kikubwa kuna vitu flani ambavyo hatujavizoea katika sehemu nyingne nyingi. Ikiwa ni moja kati ya nchi tajiri kabisa duniani ikiwa nyuma ya China na Marekani hebu tazama vitu ambavyo Japan wana vifanya tofauti na seehemu nyingine.

JE, MATAIFA YA ULAYA YANA MPANGO WA KUITOSA MAREKANI?

Suala la ulinzi na usalama ni moja ya mambo makubwa na muhimu ambayo kwa kipindi kirefu yamekua yakisumbua vichwa vya watunga sera na viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali makubwa duniani. kufuatia vitisho vya vya uliokua muungano wa Soviet ulipelekea kuundwa kwa Umoja wa kujihami wa NATO mwaka 1949 na baadae muungano wa Soviet uliunda umoja wake wa Warsaw Pact mwaka 1955.

MAREKANI YAIONYA IRAN KWA KUIWEKEA VIKWAZO VIPYA.

Image
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora. Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.

MAPINDUZI YA KIJESHI NCHI UTURUKI

Kundi moja la kijeshi nchini Uturuki linasema limechukua udhibiti wa nchi, huku madaraja jijini Istanbul yakifungwa na ndege za kijeshi zikionekana kupaa katika anga ya Ankara.

SANDERS NA CLINTON KUSIMAMA PAMOJA

Wagombea wawili wa chama cha Democrat nchini Marekani, Ben Sander na Hillary Clinton wanatarajiwa kuungana pamoja kwa kile kinachoonekana ni kujaribu kuunganisha nguvu ya chama chao dhidi ya Republican.

MARAISI WA ZAMANI KUSUSIA KONGAMANO KUU LA CHAMA CHA REPUBLICAN

BUSH Snr na Jr, Mitt Romney Kutohudhuria kongamano la chama cha Republican litakalo fanyika mwezi huu.

ETHIOPIA WAZIMA MITANDAO YA KIJAMII

Mitandao ya kijamii nchini Ethiopia imezimwa kwa sababu ya mtihani wa taifa. Waethiopia waliamka Wikiendi wakajipata hawana huduma hizo za mitandao kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber.

KOREA KASKAZINI YATAKA MAWASILIANO NA MAREKANI

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini, wanasema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.

MTOTO WA OSAMA AAPA KULIPIZA KISASI JUU YA KIFO CHA BABA YAKE.

Mwanaye wa aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.