TRUMP NA MAREKANI VS NICOLAS MADURO NA VENEZUELA, JE, VITA IKO KARIBU?
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro. Picha na Reuters Kumekuwapo na sintofahamu kubwa juu ya kile kinachoendelea kati ya Marekani na Venezuela kufuatia matendo hatarishi ya pande zote mbili. Awali Marekani ilitangaza dau nono la dola milioni 50 ambazo ni sawa na karibu sawa na shilingi 12, 529, 390, 000/= kama zawadi kwa mtu yeyote anatakaye wezesha kupatikana na kukamatwa kwa Rais wa Venezuela ambae anatuhumiwa kwa ulanguzi wa madawa ya kuelevya. Lakini hilo limechukua sura mpya baada ya Marekani kutuma meli za kivita pamoja na nyambizi karibu na Venezuela kitu ambacho kimemlazimu Rais Maduro kuanza kukusanya wanajeshi wakijiandaa kwa makabiliano ikiwa Marekani itawavamia.