Saturday, 9 July 2016

FACEBOOK KUTUMIKA KUTUMA NA KUPOKEA PESA.

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni na hayawi hayawi sasa yamekua.

WATU 12 WAFARIKI KWENYE FOLENI

Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha.

UNATAKA KUFUTA TAARIFA ZAKO KUTOKA GOOGLE? USIPITWE NA HII HAPA.

Ulishawahi kukaa ukafikiria kama unahitaji kufuta taarifa zako kutoka Google? Sasa usiwaze kila kitu ni kirahisi. Labda ulishawahi kutumia Google kutafuta taarifa flani na

Friday, 8 July 2016

KAMA UNAMILIKI SMARTPHONE NA UNAPENDA KU EDIT PICHA HAKIKISHA HAPITWI NA HII

Kama unamiliki smartphone au kompyuta na unapendelea kuhariri picha zako basi moja kati ya hizi application za kuhariri picha sio za kukosa!! Unaanzaje kukosa kwa mfano??

TOP 10 YA VIONGOZI WANAOTUMIA MAGARI YA BEI MBAYA KULIKO




Inaendelea.....

Haya magari ntatoa baadhi ya sifa zake kwa ufupi.

PILISI WANNE WAUWA NA SABA KUJERUHIWA

Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Thursday, 7 July 2016

ZIJUE NCHI AMBAZO VIONGOZI WAO WANATUMIA MAGARI YA BEI MBAYA KULIKO

Maisha ni kuchagua na kuchagua ni kupanga wenzetu walichagua. Wafalme, malkia, maraisi na masultani wanachagua wanachokitaka. Hapa nina orodha ya

MAREKEBISHO MADOGO KWENYE UTEUZI WA WAKURUGENZI WAPYA.

Taarifa iliyotolewa na ikulu hivi punde ni kua imefanya marekebisho kidogo kwenye uteuzi wa mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma. Soma hapa>>http://lm.facebook.com/l.php?u=http%3A%2F%2Fmillardayo.com%2Fikulu54%2F&h=DAQEVAVqM&enc=AZOUxU6N-bqy1D41_Cj46xwFkxGijdqoPMrLC671vLcOeP2AKa745THKGyaXdUWfIOHLXyORPW8CRMptd1Xuy3nduL9A5T6LJ6HpSEcGpVyrs-tHvRD8RhmVvxaIBD2cOPGs-7_6r1HgxdbGIaRpG2dP60ED9bSnsU3sHDIiTF_FQBDs6fU_FChELx3R2mU-nPE&s=1

WAKURUGENZI WAPYA

Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa leo na Rais Magufuli
Newsroom TZA

POLISI NCHINI MAREKANI WAMEMUUA MMAREKANI MWEUSI

Mtu mwingine mweusi amepigwa risasi na kuuawa mapema leo na polisi wa trafiki katika jimbo la Minnesota Marekani.

WACHEZAJI WANAPCHUKIWA ZAIDI DUNIANI KWA SASA

Mtandao wa Goal.com umetoa orodha ya wachezaji wanaochukiwa zaidi katika historia ya soka.

MANISPAA YA IRINGA YANG'ARA NG'ARING'ARI


Manispaa ya iringa imeibuka idedea kwenye swala la usafi kitaifa. Manispaa hio imeipiku manispaa ya moshi ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikiongoza kwa usafi.

DONALD TRUMP AMSIFU SADDAM HUSSEIN



Wakati watu wengi wa marekani wakiamini kua Saddam Hussein alikua ni dikteta wa Iraq na mtu aliye fadhili ugaidi hali ni tofaututi kwa Trump.

MESSI KUTAKA RUFAA KUPINGA HUKUMU YA KESI YAKE

Wanasheria wa mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi pamoja na baba yake Jorge Messi wanatarajia kukata rufaa kupinga

Wednesday, 6 July 2016

NGUVU YA MJINGA HAIDHARAULIWI.

Usiidharau nguvu ya wajinga kwa maana wakiungana wana nguvu kubwa ya kuamua hata kama ni maamuzi ya kijinga.

ORODHA YA MABILIONEA WAKUBWA KWA MWAKA 2016 TANZANIA YUPO MMOJA TU.

Wakati tunaendelea kulalamikia ugumu wa maisha lakini upande mwngine hali ni tofauti. Ukweli n kwamba uchumi umekua mgumu kwa kila mtu, ila hii hapa ni orodha ya mabilionea wa Afrika mwaka 2016.

Mabilionea hawa wana utajiri wa pamoja unaofikia $80.94bilion ikiwa

RAISI OBAMA AMPIGIA "DEBE" WAZIRI WAKE WA ZAMANI.

Raisi wa marekani Barack Obama amefanya kampeni na aliyekua waziri wa mambo ya nje

MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA DAVID CAMERON WAANZA.

Conservative wapiga kura ya mrithi wa Cameron

Mchakato huo wa Kura unafanyika wakati ukiongezeka wasiwasi kuhusu taathira za kiuchumi baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

UNAJUA KUFANYA HAYA UKIWA NA SMARTPHONE YAKO? FANYA VINGI NA VIKUBWA UKIWA NA SMARTPHONE.

Unatumiaje "Simu janja" yako? Inawezekana ni mtumiaji mzuri wa smartphone lakini kuna "features" kwenye simu yako hukuwahi kujua kama zipo na labda pengine hufahamu kama simu yako inaweza kufanya jambo flani.

Kila mtu anajua jinsi ya
kutumia smartphone japo wengi wetu tumeanza kutumia smartphone bila kusoma "User Manual" na hivo kushindwa kuitumia simu hadi kiwango chake cha juu cha matumizi. Hivi ni baadhi ya ambavyo wengi hawajui jinsi ya kutumia.

1. UNA UWEZO WA KUPIGA PICHA 10 KWA SEKUNDE.ULISHAWAHI KUFANYA HIVI??  Ndio picha 10 ndan ya sekunde moja! Iko hivi kama wewe unatumia android fanya hivi;
Fungua camera yako > bonyeza kitufe cha "settings" kisha weka "Burst shot ON"(unaweza kutumia pia button ya kuongeza na kupunguza sauti)>> kisha kandamiza(gusa bila kuachia) "Shutter button" hadi utakapoona inatosha au hadi simu itakapofika idadi ya mwishi ya kuchukua izo "continuous pics". Nadhani umeelewa sasa unaweza kuchukua picha 100 nda ya sekunde 30 tu!! Jaribu sasa!!

2. UMECHOKA KUSOMA VITU VILIVYOPO KWENYE SIMU??

Usihofu fanya hivi....
Washa simu yako nenda kwenye "settings" kisha>> Accessibility na bonyeza "TalkBack". Kama hicho kitu hakipo kwenye simu yako nenda kakipakue Play store. Baada ya hapo rudisha simu yako kwenye home screen na simu itasoma chochote utakachokibonyeza pamoja na taarifa zinazoingia. Ili kuweza "Ku swipe" simu yako tumia vidole viwili badala ya kimoja.
Kama hupendi jinsi simu inavyoongea unaweza kubadili sautu na speed kwa kwenda kwenye "Settings" >>>Accessibility >>>text-to-speed options na badili sauti na speed. Na kisha nenda kwenye "Settings" na uweke "Hands-free mode" ili simu iweze kutambua anaekupigia na kukutumia ujumbe.

3. KU BLOCK TEXT NA SIMU YA MTU AMBAE HUTAKI AKUPIGIE AU AKUTUMIE UJUMBE.

Nenda kwenye "Settings" >>>Call settings >>>chagua Incoming calls na bonyeza call block list >>>create. Apo utaingiza namba ya mtu unaetaka asikupate, kama huna kichwani bonyeza kwenye alama ya picha unayoiona kwenye screen yako kisha itakupeleka kwenye phone book au call history na uko utachagua namba ya muhusika.
Ila unaweza kumtoa mtu kwenye kifungo hiki.

Nadhani umeongeza maarifa juu ya kutumia smartphone yako na kama unakitu hukielewi unaweza kuacha comment yako hapo chini au kwenye ukurasa wa facebook. Tukutane wakati mwingine bye byee!!!

Tuesday, 5 July 2016

FBI WATOA TAARIFA YAO YA UCHUNGUZI DHIDI YA HILLARY CLINTON

HILLARY CLINTON KAKALIA KUTI KAVU??

FBI wametoa taarifa yao ya uchunguzi juu ya tuhuma zinazo mkabili mgombea wa wa uraisi wa marekani kupitia chama cha Democrat,

DONALD TRUMP NA MAREKANI MPYA(Muendelezo)

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya marekani(muendelezo...)

KWA MARA YA KWANZA KABISA SAYARI YA JUPITER (ZOHALI) KUFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA.

NASA imetoa taarifa kua chombo chao cha JUNO kilichotumwa mwaka 2011 kewasili mapema leo asubuh na kuanza kazi yake ya kuizunguka sayari hio. NASA  wanatarajia kukitumia chombo hicho hadi mwezi February 2018. Kwa maelezo zaidi soma hapa..>>>http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160704_juno_spacecraft

TUIGE MFANO WA ETHIOPIA.

Licha ya changamoto za ukame zinazo ikumba Ethiopia lakini bado wana nia ya dhati ya kuifanya Ethiopia kua taifa  na lenye nguvu kiuchumi barani Afrika.

Taifa lolote ambalo lina watu makini, viongozi wenye mawazo ya mbali, waadilifu na waliojitoa huweza kuendelea kwa haraka zaidi kuliko inavodhaniwa.

RAISI MAGUFULI ATENGUA NA KUTEUA WENGINE.

Raisi magufuli afanya mabadiliko kwenye benki ya TIB

Taarifa niliyoipokea kutokea ikulu inasema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria

MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA KUCHUNGUZWA DAR.

Ndege iliyopotea Malaysia kuchunguzwa nchini


Florence Majani
Bawa mojawapo la ndege hiyo linadaiwa kupatikana hivi karibuni katika Kisiwa cha Kojani,

DONALD TRUMP NA MAREKAMI MPYA.

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya Marekani.

1. Wamarekami wengi wenye asili ya kiarabu walishangilia lile shambulizi la september 11 2001. Hili ni shambulio baya kabisa kwa nchi ya marekani miongo kadhaa.

2. Anaamin kua miskiti yote nchin marekani inapaswa

PANYA WA SUA KUPIMA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU ETHIOPIA.

Panya wa Sokoine kutumiwa Ethiopia

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nchini Tanzania wanapanga

Monday, 4 July 2016

NATO na Urusi "Kupooza" Mvutano.

NATO na Urusi kufanya mazungumzo ya pamoja baada ya kilele cha mazoezi ya kijeshi huko Warsaw.

NATO and Urusi watafanya mazungumzo rasmi mara  baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kijeshi mjini Warsaw wiki hii.

NI JEURI YA PESA AU KIBURI??

Klabu ya Manchester united ya uingereza imesisitiza kua inataka kumsajili tena kiungo wa ufaransa na

DHIMA YA KITABU CHA REPUBLIC (2)

#REPUBLIC_SEHEMU_YA_2

Baada ya kukubaliana maana hak na katba Socrates aliamua kueleza kuhusu katba isiyo hak. Lakin anaanza kwanza kutueleza n vp mtawala "philosopher king"

HASIRA ZAONGEZEKA MIONGONI MWA WAKAZI WA BAGHDAD.

Kufuatia shambulio la kigaidi la lililotekelezwa na kikundi cha ISIL na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200 wengi wao wakiwa n watoto kimeamsha hasira miongoni mwa wakazi wa Baghdad wengi wao wakiilaumu serikali ya Iraq kushindwa kuwalinda.
Shambulio hilo la mapema jumapili limesababisha tafrani kubwa miongoni mwa wananchi wa Baghdad kwa kua licha ya  serikali kutangaza kuukomboa mji wa fallujah ambao ulikua n ngome muhimu kwa ISIL  lakini bado haijaweza kuhakisha kua maeneo yote ya Iraq yanapata ulinzi wa kutosha ili kukabiliana na wanamgambo wa ISIL.

RETHINK and then REWRITE

Ukiisoma hii article ni kama unamsikiliza mwanamapinduzi wa kiafrika!! https://www.africanexponent.com/post/history-of-europeans-in-africa-is-not-african-history-3231

UINGEREZA KUPUNGUZA KODI KWA MAKAMPUNI.

Uingereza kuvutia makampuni ya biashara

Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake yenye lengo la kupunguza kodi muhimu ya faida katika biashara.
Hatua ya Osborne ni sehemu ya mkakati wa kiuchumi katika harakati za kuvutia uwekezaji mpya, na hii inafuatia kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo iliamua Uingereza isite kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya.
Osborne aliliambia gazeti la Financial Times kwamba anataka kupunguza kodi ya shirikishi kutoka asilimia ishirini hadi chini ya asilimia kumi na tano.mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara ameeleza kwamba kura ya maoni ilikuwa ni mkakati wa kuisaidia Uingereza kuvutia uwekezaji kutoka kwa kampuni mbali mbali mpango ambao inawezekana haukufanikiwa kufuatia kura hiyo ya maoni.

UNADHANI TATIZO LA AJIRA NI LAKO PEKEE?

Kuna msemo husema kua "kukimbia tatizo sio njia ya kulitatua". Huyu jamaa alikimbia kwao na kwenda kusaka kazi CHINA na hii ni story alotuletea.
https://m.facebook.com/l.php?u=https%3A%2F%2Fwww.africanexponent.com%2Fpost%2F7480-is-the-grass-greener-on-the-other-side-of-the-fence&h=6AQEihDi2&enc=AZPfcmQcb3iBfAxSuYjDfJr2aabJTy-LyTeVnCPZGNDpytp3OuRDUXNcsaoQ-gO03tU69DwuBSHfxh8BJ39pRv525qGKjc5fe5S-vvu1RXj3cxQEvBD9rhdcQk5FdHzTkvL4NrqsU0R6vX1Oo4ERZouVtKPvyXhFwCrhb8ptPvcgh-1BQC9wHULFyuUwX4v-h2I&s=1

TAZAMA MIMEA HII NA UTAJIFUNZA KUA KATIKA MAISHA HAKUNA KUKATA TAMAA.

Inawezekana unaona maisha ni magumu saana na huna budi kukata tamaa. Lakini kila siku amini kua neno "Nimeshindwa au Siwezi" halipo katika dunia yako.

Tazama picha hizi kumi ambazo zinakuonesha kua kuna uwezekano wa maisha "kutokeza" popote utakapoamua kutokea. 

https://www.africanexponent.com/post/7478-10-plants-which-conquered-death

MAUDHUI YA JUMLA YA KITABU CHA REPUBLIC [PLATO]

WAKATI FLANI NI VEMA TUJIHUKUMU WENYEWE NA BAADA YA HUKUMU TUJIADHIBU KWANZA KABLA HATUJAADHIBIWA. KATIKA MAISHA KUKOSEA KUPO LAKINI NAFAS YA KUJISAHIHISHA PIA IPO PALE PALE.  UONGOZI NI MAISHA YA MAKOSA LAKIN LAZMA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA YETU. HUWEZI KUA BORA PASIPO KUKOSEA. 

#REPUBLIC ni moja kati ya vitabu maaruf saana duniani. Kiliandikwa na Mwanafalsafa nguli #PLATO yapata takriban karne 4K.K (Kabla ya Kristo). Kitabu kimeshehen mazingumzo ya wanafalsafa nguli akiwemo #Socrates ambae pia ni mwalim wa #Plato. Kitabu hiki kinaeleza maana ya HAKI, utawala wa hak na hak ya mtu. watu weng wakiongozwa na Socrates waltoa maana ya hak kua n kutoa kile unachodaiwa,

FALSAFA YAKO NDIO INAKUONYESHA WEWE UKO VIPI NDANI

Falsafa ya "TOTAL FOOTBAL"


MCHEZO HUU HAUHITAJI HASIRA WALA UBABE. 

Unajua huwa napenda sana jins ambavyo FC Barcelona hua inacheza. Mfumo huu uliàasisiwa huko Uholanzi na mfumo huu uliletwa na Johan Cruyff pale FCB(yeye alikua akiutumia kwenye team yake ya Ajax na ile ya taifa). Katika mfumo huu kila mchezaji anapaswa kuchangia katika upatikanaji wa goli na unaruhusu mchezaji mwingne kuchukua nafasi yà mwenzake mkiwa mchezon.

JOINING INSTRUCTIONS

PAKUA HAPA FORM ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2016 KWA SHULE ZOTE.

http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/joining-instructions

ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2016

Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa orodha majina ya kidato cha tano 2016

http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/

MWALIMU HUYU ATSTUFAA SISI WANAFUNZI?

Kaspersky: *SHULE SERIES* *HEAD MASTER/ MWALIMU MKUU* *SEHEMU YA KWANZA* Nakumbuka kwa uzuri kabisa kua siku hio ilikua n nzuri saana, maama niliamka asubuhi na mapema nkavaa sare zang mpyaaa za shule yetu, nilibeba mfuko wangu wa madaftar...na safar ikaiva kwenda kuanza shule rasmi! Nilipofika shule nilipokelewa kwa tabasamu za walimu na wanafunzi pale shuleni. Kila mtu alifurahi kwa kua mda mfupi ndipo shule yetu ilikua imeanzishwa kwa juhudi za mkuu wa shule bwana Rev.Democrat. Kwa kweli mkuu wetu alipendwa saana kutokana na juhud zake za kuipigania shule kwa maslah ya watoto pale kijijin na vijiji vingne vya jirani. Lakin sio km watu wote walikubaliana nae la! Wengne walimpinga. Kutokana na uchanga wa shule tulisoma kiugumu ugumu ila mkuu mara zote alisisitiza kuthubutu, kujiamin na kujitegemea. Kwa kweli ndoto yake ilikua n kuleta usawa na maendeleo kwa kila mtu lakin haikua kaz rahis, alifanikiwa kwa kias chake lakin sio km alivyoota kua ije kua. Miaka ilipita shule isonga mbele japo changamoto zilikua nying mwalim mkuu alijarbu kuzitatua kwa kutumia *akili, busara, utashi, weled na maarifa*. Alihimiza kujitoa kwaajili ya wengi. Nakumbuka siku moja alitukusanya wanafunzi na wazaz/walez akisema kuna jambo alitaka kutuambia.😥😢 Tulifika kwa wingi na kama ilivo ada tulikua na furaha ila baada ya muda mfup hapakua na furaha hata kidogo😢😥, nakumbuka tulikua tumejiinamia hakuna mtu aloweza hata kunong'ona ndipo nilisikia sauti kutoka mbaaal zikijisifia kua *"Tumeshinda! Tumesjinda"* zikiambatana na vicheko vya kejeli. Mwalim mkuu alituambia kua hawez kuendelea kuiongoza shule yetu. Hiki ndicho kilileta huzuni😥. Ningali najiuliza saana juu ya zile sauti na vicheko ni za akina nani? 😳 **~~~** Siku zilienda mwishowe tukampata *Mwalimu mkuu Mpya* huyu mkuu hakua km yule mwanzo😥🤔 aliamuru shule yetu iandikishe mtoto yeyote bila kujali atokapo. Nakumbuka siku moja tulikua darasani tukiwa tumejazana saana kwa bahat mbaya mwanafunzi mmoja akajamba! Hali ya hewa ibadilika ikawa mbaya mno tukasukumana na kupiga kelele labda kila mtu avute hewa ya *Oksijeni* japo mara moja😢🤔. Mwalimu mkuu baada ya kuona vile akaamuru tufungue madirisha. Kwa kua darasa letu lilikua ule upande wa choo cha wanafunzi basi *NZI* walimiminika darasan na tuliposema *"Jaman fungeni madirisha!"* mkuu akasema *"Msifunge madirisha kwan nzi wakiingilia upande huu wa kulia watatokea kushoto"*. Niliguna kwa sauti mkuu akageuka na kuniambia *"Nimefanya hivi ili tupate kupumua, tumia mkono na daftar lako kufukuza nzi ila hatutafunga madirisha"*😥😳 Namkumbuka mwali huyu km Mr.FreeAir. Hakukaa muda sana akaja mwingne... (Bado nipo shule) *Itaendelea....*