Friday, 14 December 2018
ZINGATIA HAYA KABLA YA KUNUNUA SMARTPHONE YAKO.
DONDOO MUHIMU KABLA YA KUNUNUA SIMU MPYA.
Kwa sasa kuna makampuni mengi yanayozalisha simu na simu hizo kila ile ni bora kwenye nyanja flani na wakati mmoja zinaweza kua bora nyanja zote. Ili kuepuka kununua simu mara kwa mara na kulinda kipato chako unaweza kufanya yafuatayo.
1. Angalia mfumo endeshi wa simu (Operating system) unaweza kuchagua Android au IoS kulingana na mahitaji yako mwenyewe au matakwa ninafsi. Kila mfumo endeshi una faida na hasara zake kwa hio ni vema kuchunguza kwanza kabla hujaingia dukani.
2. Angalia features muhimu za simu husika.
Usiende tu kununua simu ila uwe na vigezo nanunua simu hii kwa sababu flani. Mfano kwa simu za sasa nying zinakua na fingerprint scanner, face ID, AI technology n.k kama unapenda kwenda kisasa lazma ujue je, simu ina hizo features?
3. Ufanisi na uwezo wa simu.
Utaipima simu kwa kuangalia uwezo wake wa kufanya kazi mfano kufungua mafaili, ubora wa picha na video, urahisi wa kucheza game, ukubwa wa memory n. k. Mfano ili kua na uhakika kwa kuhifadhi taarifa nying utahitaji kua na simu yenye 16 GB ROM, na ili kufanya simu iwe nyepesi katika utendaji walau RAM ya 2 na kuendelea itakufaa. (Hii ni kwa mtumiaji mdogo). 4. Muundo wa simu na muonekano.
Chunguza materials zilizotumika kuunda simu hasa seem ya nje ya simu na muonekano wa jumla wa simu yenyewe. Muundo mzuri ni ule unaorahisisha ushikaji wa simu hasa wakati wa kuitumia.
5. Chunguza suala la bei kwanza.
Kila kitu kizuri kinakua gharama lakini unaweza kupata kitu kizuri kwa gharama ya kawaida kabisa. Usikurupuke kununua simu bali fanya uchunguzi kwanza kujua hali ya soko na range ya bei za bidhaa kama hio.
Wakati mwingne ntakuandikieni namna ya kulinganisha teknolojia iliotumika kutengeneza, uwezo na ufanisi wa simu.
Usisahau kuwa tag washkaji zako unaohisi wanapaswa kujua hizi dondoo.
Kujua zaidi na mengine ufuate ukurasa wetu wa Instagram @xmarttech
#xmarttech
#WeLiveTheFuture.
#smartTechnologies.
Subscribe to:
Posts (Atom)