Posts

Showing posts with the label MAONI & UCHAMBUZI

TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?

Image
TRUMP VS PUTIN NANI MBABE WA MWENZAKE?   Rais wa Marekani Donald Trump akiongea jambo na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin baada ya mkutano wao huko Alaska 15 Agosti 2025/ picha kwa hisani ya Ikulu ya Marekani   Rais wa Marekani Donald T rump na Rais wa Urusi Vladimir Putin ni miongoni mwa majina makubwa katika medani ya siasa za kimataifa kutokana na hulka yao na namna wanavyochukua maamuzi magumu katika nyakati ngumu. Na hivyo kufanya dunia kua na viongozi shupavu kama wanne hivi kwa maana ya nyongeza ya Xi Jin Ping wa China pamoja na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini. Ila kwa sasa ni Trump dhidi ya Putin wakikaa wawili nani mbabe wa mwenzake? 

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU

Image
  'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU K atika ulimwengu wa kijasusi mambo mengi hutokea na wakati Fulani hivi ni ngumu kuamini kama hayo yanayotoka katika ulimwengu huo ni kweli au ni stori za kufikirika. Naam, ni takribani  miaka 50 sasa tangu Israel ilipopata taarifa za shambulio katika ardhi yao ndani ya saa 24 kabla ya tukio kutoka kwa “ANGEL” kwa maana ya “MALAIKA”. Ambapo bila taarifa kutoka kwa huyu "the Angel" kusingekua na Israel na kama ingekuepo basi ingekua tofauti sana na iliyopo sasa. 

ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?

Image
Picha kwa hisani ya mtandao ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?  "Vita havina macho". Ni msemo tu katika jamii nyingi ukiwa na onyo la kutokushadadia vita.  Tarehe 7 Oktoba 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi kwa saa za Israel, kulitokea shambulio la kushtukiza kutoka kikundi cha HAMAS ambacho kwa tafsiri ya Marekani na washirika wake ni kikundi cha kigaidi.  Tukio hilo lilidhihirisha udhaifu katika idara ya ujasusi ya Israel kwa maana ya Mosad pamoja na Shin Bet. Kikubwa zaidi ni kile kilichokuja kuwa ni kisasi cha Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza. Itoshe kusema mitaa mingi ya Gaza City imekua kama mji wa Kale uliokumbwa na kisa cha kutisha mno. Imekua kama "Ghost City".  Tangu hapo kumekuwa na maoni tofauti juu ya nani yuko sahihi katika hili. Ukweli ni kwamba katika wakati huu ni swali baya ila kikubwa ni nani atasalia? Achilia mbali kua sahihi. 

CHINA NA MAREKANI: HISTORIA, UHASAMA NA TISHIO LA DUNIA-2

Image
Volume 1 Issue 2 [Muendelezo] 2023/0/25  Rais wa China Xi Jin Ping (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kuliko) China ni Taifa Jeuri na Kiburi Cha Kimya. Ikiwa tunapaswa kuelewa majibu ya China dhidi ya Marekani basi hatuna budi kuangalia hatua mbalimbali ambazo Marekani iliwahi au imezichukua dhidi ya China katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Lakini tutaangazia zaidi hatua zilizochukuliwa katika miaka ya hivi karibuni. Bado ni hoja nyepesi kusema kinachoendelea kati ya Marekani na China ni muendelezo wa vita baridi labda kwa asiyeifahamu vita baridi. Ilikua inatisha kuliko jina lake la ‘vita baridi’. Kuna mambo kadhaa yameweka reheni mahusiano ya China na Marekani na ni muhimu kuyaangazia kiasi.

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY. Kwanza nipende kuwapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo naona swala la teknolojia ya habari na mawasiliano limeweza kua ni chachu ya mabadiliko hapa nchini. Na kama tutaendelea kua na weledi wa matumuzi bora ya maendeleo haya ya sayansi na teknolojia basi, naamini tutafika mbali. **