OPEN AI YAMKAANGA ELON MUSK NA MARK ZUCKERBERG HUKO MAHAKAMANI
Sam Altiman muanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Open AI. Picha na AFP na Getty Images Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali nchini Marekani zinaonesha kua kampuni ya Open AI ambayo inamilki ChatGPT imetoa maelezo mahakamani kua tajiri namba moja duniani Elon Musk alijaribu kumshawishi hasimu wake kibiashara Mark Zuckerberg ambae ni mmiliki wa kampuni kubwa ya Meta (Facebook, Instagram, WhatsApp na Thread) ili wachanhiane au waingie ubia katika uwekezaji wa kuinunua Open AI ambapo Elon Musk aliweka dau la dola za kimarekani bilioni 97.4, hata hivyo kulinga na Open AI Zuckerberg hakua ameafiki hilo.