HISTORIA YA UBAGUZI WA RANGI AMERIKA
(MAREKANI)
Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha/imani ya
kumbagua/kumtenga/kumchukia mtu kwa misingi ya asili yake na rangi ya ngozi
yake. Hii sio kitu kigeni sana na ni vigumu kusemea kirahisi ni lini hasa
ubaguzi wa rangi ulianza hasa kabla ya karne ya 15. Wakati wazungu wanakuja
Afrika kwa mara ya kwanza kutoka Ureno (Portugal) walidhan kua Waafrika ni
jamii hasimu kwao kwa maana ina uwezo sawa na wao lakini punde wakajua waafrika
walikua dhaifu kwenye baadhi ya maeneo na hapo waafrika wakaanza kuchukuliwa
jamii dhaifu (Inferior race). Hali hii ndio iliopelekea kuzaliwa kwa biashara
haram na ya kishenzi_biashara ya utumwa.