SAWA, HATIMAE MUGABE AKUBALI KUJIUZULU.
Kwa mujibu wa taarifa ya CNN imeripoti kua chanzo rasmi kinachofuatilia mazungumzo kati ya rais Mugabe na maafisa wa jeshi kimedokeza kua rais Mugabe amekubali kujiuzulu kufuatia hatua ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo kumuweka kizuizini kwa siku kadhaa. Hatua hii inakuja kufuatia hatua yake ya jana jumapili ambapo kwa mara ya kwanza tangu awekwe kizuizini nyumbani kwake alilihutubia taifa kupitia shirika la utangazaji la nchi hio ZBC.