Friday, 14 October 2016

NCHI ZINAZOONGOZA KWA AMANI AFRIKA.


Kulingana na Global peace index 2016 wametoa orodha ya mataifa yanayoongoza kwa amani duniani. Nchi hizi zimepangwa kulingana na viashiria vikubwa vitatu: kiwango cha ulinzi, usalama na kiwango cha migogoro ya ndani na nje ya nchi na pia nguvu za kijeshi.

Thursday, 13 October 2016

MWANAFUNZI ATENGENEZA BOMU LA MACHOZI,

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda amevumbua njia ya kutengeneza mabomu ya kutoa machozi ambayo hutumika na vikosi vya Polisi mara nyingi kuzima maandamano.

Tuesday, 11 October 2016

JENGO LA JULIUS NYERERE LAFUNGULIWA RASMI ETHIOPIA.


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Julius Nyerere.

Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.
Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).

Monday, 10 October 2016

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.

Kwanza nipende kuwapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo naona swala la teknolojia ya habari na mawasiliano limeweza kua ni chachu ya mabadiliko hapa nchini. Na kama tutaendelea kua na weledi wa matumuzi bora ya maendeleo haya ya sayansi na teknolojia basi, naamini tutafika mbali. **