JE, MATAIFA YA ULAYA YANA MPANGO WA KUITOSA MAREKANI?
Suala la ulinzi na usalama ni moja ya mambo makubwa na muhimu ambayo kwa kipindi kirefu yamekua yakisumbua vichwa vya watunga sera na viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali makubwa duniani. kufuatia vitisho vya vya uliokua muungano wa Soviet ulipelekea kuundwa kwa Umoja wa kujihami wa NATO mwaka 1949 na baadae muungano wa Soviet uliunda umoja wake wa Warsaw Pact mwaka 1955.