Friday, 15 December 2023

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU

 

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU


Katika ulimwengu wa kijasusi mambo mengi hutokea na wakati Fulani hivi ni ngumu kuamini kama hayo yanayotoka katika ulimwengu huo ni kweli au ni stori za kufikirika. Naam, ni takribani  miaka 50 sasa tangu Israel ilipopata taarifa za shambulio katika ardhi yao ndani ya saa 24 kabla ya tukio kutoka kwa “ANGEL” kwa maana ya “MALAIKA”. Ambapo bila taarifa kutoka kwa huyu "the Angel" kusingekua na Israel na kama ingekuepo basi ingekua tofauti sana na iliyopo sasa. 

Wednesday, 13 December 2023

BILA HAWA WATANO KUFA, ISRAEL HAIWEZI KULALA GAZA

 
Moshi mkubwa baada ya kombora kupiga sehemu ya majengoya Gaza

NETANYAHU HAWEZI NA IDF HAIWEZI KULALA KAMA HAWA BADO WAKO HAI

Ni zaidi ya miezi miwili tangu Oktoba 7 ambapo wanamgambo wa HAMAS waliweza kuvamia kusini mwa Israel na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu na kibinadamu na kugharimu maisha ya zaidi ya Waisrael 1200 huku wengine zaidi ya 240 wakichukuliwa mateka mpaka ukingo wa Gaza.

Benjamin Netanyahu a.k.a Bibi awali alivikosoa vikosi vya jeshi la Israel kwa kushindwa kuzuia shambulio hiilo baya ana la aibu kwa Israel lakini baadae aliomba radhi na ujumbe wake huko X (zamani Twitter) ukaondolewa. Netanyahu aliapa kwamba Israel italipa kisasi juu ya tukio hilo na kwamba Hamas watalipa gharama kubwa na kwamba ni lazima kundi la HAMAS liangamizwe kabisa. Je kauli yake inawezekana? Umeskia nini kuhu Isarel? Inalindwa lakini unajua nini kuhusu HAMAS? Ni kikundi cha magaidi au ni zaidi ya hapo? Fuatilia kwa makini…