Rais wa marekani (kushoto) na rais wa korea kaskazini(kulia).
UJUE KWA UNDANI UHASAMA WA MAREKANI NA KOREA KASKAZINI.
Siku za hivi karibuni kumeibuka mvutano mkali na vitisho baina ya mataifa hasimu kihistoria moja kutoka rasi ya korea na jingine kutoka amerika ya kaskazini. Mvutano huu umeongeza hofu ya kutokea kwa vita ya tatu ya dunia na imechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kila mahali. Lakini wengi hatufahamu hasa kwanini mataifa haya yamekua hasimu kwa kipindi kirefu na labda ndio uhasama mkali zaidi duniani. Maelezo haya yatakusaidia kuelewa kwa undani uhasama huu.
HISTORIA FUPI YA UHASAMA.
Mataifa haya mawili yamekua katika uhasama kwa karne kadhaa. Na hakujawahi kua na uhusiano wa moja kwa moja wa kidiplomasia baina ya marekani na Korea kaskazini. Mnamo karne ya 19 Marekani alitaka mahusiano ya kibiashara na korea lakini korea walikataa japo baadae walikuja kukubali. Tangu zamani Marekani ilionekana kama taifa lisilo haki mbele ya Korea. Wakati karne ya 20 uhasama huu uliongezeka zaidi baada hasa baada ya Japan kuingilia kimabavu na kuitawala Korea tangu mwaka 1910-1945. Katika kipindi hiki Korea waliitaka Marekani iwasaidie kuung'oa utawala wa kimabavu wa Kijapan lakini Marekani alisimama upande wa Japan kuplingana na maslahi yake.
Mwaka 1945 Urus ilikusudia kuidhibu Japan na iliyasaidia majeshi ya Korea kumuondoa Japan na hivo Korea kua taifa huru japo uhuru huu haukutambuliwa na mataifa ya kimagharibi.
Uhasama uliongezeka mara dufu baada ya vita vya Korea 1950-1953. Kipindi hiki Marekani alipigana upande wa Korea Kusini mwanzo mpka mwisho wa vita na baada ya vita Marekani iliacha majeshi yake kule ili kuendelea kuilinda Korea Kusini. Hiki kitendo kiliiudhi na bado kinaendelea kuiudhi Korea ya kaskazini ndio maana uhasama wao sio rahisi kuisha. Tangu wakati huo kiongozi wa Korea kaskazin Kim Il Sung aliamini adui namba moja duniani ni taifa la kibepari la marekani na marekani aliamin Korea kaskazin ni taifa la kishetani.
Kuanzia pale Korea kaskazini imekua ikijihami dhidi ya uvamizi wa Marekani na hivyo ili kujilinda waliamua kuanza programu yao ya kutengeneza silaha za nyuklia. Hiki kitendo kiliwakera na bado kinawakera sana wamarekani kwani silaha hizi ni mataifa manane tu yanazo hapa duniani. Na wengi n washirika wa marekani kasoro RUSSIA na CHINA. Kwa kuhofia kua siku moja Korea akimiliki silaha anaweza kuipiga Marekani au silaha zile zikaangukia mikononi mwa makundi ya kigaidi marekani hutumia vitisho kuidhibiti Korea au vikwazo vya kiuchumi, lakin Korea haijawahi kutishika.
Kuanzia 1968-1976 mengi yalitokea ikiwa ni pamoja na kudunguliwa kwa ndege ya marekani, kukamtwa kwa cptain na lieutenant wa marekani n.k
Katika kipindi cha miaka ya 1980-2003 kulikua na vipind vifupi vya majadiliano kuhusu korea na marekani lakin hapakua na muafaka mzuri. Mwaka 2002 rais wa marekani wakati huo Bw.George Walker Bush akiwah kusema kua Korea kaskazini ni 'mhimili wa shetani' kauli ambayo iliiudhi Korea.
Kuanzia mwaka 2003 mpka sasa kumekua na mvutano mkali na hasa baada ya kifo cha Kim Jong Il ambaye ni baba wa Kim Jong Un mwaka 2011. Korea kaskazini ilianza rasmi majaribio ya silaha za nyuklia mwaka 2006. Kitendo kinacholaumiwa na jumuiya ya kimataifa na marekani pia.
Hii ni hitoria ya uhasama na mivutano baina ya korea na Marekani. Lakini vitisho vya hali ya juu na kudora kwa usalama kumekuja hivi punde mwaka 2017 wakati Marekani ikiwa chini ya utawala mpya inasema 'zama za uvumilivu wa kijeshi kwa korea kaskazini ziklmekwisha'. Je,ni kweli zimekwisha?? Usikose mfululizo wa makala ijayo itakayoangazia Korea chini ya Kim jong Un na Marekani chini ya Donald Trump na pia uwezekano wa vita ya tatu ya dunia.
Usisahau ku share na wenzako.
umeeleza vizuri ila jaribu kudesign vizuri wrtting style na uwiano wa background color na text color vinasababisha ugumu kwa msomaji
ReplyDelete