WAAFRIKA WAUNGANA NA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA NCHI GHANA. UMAJUMUI WA AFRIKA UNAPATA NGUVU MPYA?
![]() |
| Moja kati ya bango likiwa na ujumbe kua "HATUDAIWI, HATUTOLIPA" |
Bara la Afrika ni moja ila ikiwa Waafrika ni wamoja ni swali pana sana na inaweza kua vigumu kufikia hitimisho la pamoja. Wakati wa Karne ya dhahabu kwa nchi za kiafrika naweza kusema ilikua ni kipindi cha miaka ya 1960s. Hapa tulishuhudia miito mbalimbali ya Waafrika kuungana na kua wamoja au kitu kimoja na mwaka 1963 viongozi wa nchi huru za Afrika walifanikiwa kuunda Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) lakini baadae mwaka 2002 Umoja wa Afrika (AU) ulianza rasmi baada ya Sirte declaration kule Linya mwaka 1999.
Lengo lilikua ni kuwaleta Waafrika pamoja na kupigania haki na usawa katika nyanja za kimataifa. Kupitia mikutano na makongamano mbalimbali imekua dhahiri kua Afrika ina hitaji ukombozi mpya kwani sasa inaelekea kulekule tuliko toka kwenye miaka ya 1980s ambapo madeni ya nje yalizidhoofisha nchi za kiafrika na kufikia hatua ya kufilisika ndipo taasisi za kifedha za kimataifa na nchi wakopeshaji zikaja na kifurushi cha sera za mageuzi ya kimuundo, kiuchumi na kifedha maarufu kama Structural Adjustment Program (SAPs) ili kuwezesha mataifa maskini kukopa mikopo kulipia madeni ili waweze kukopesheka tena. Hili ndilo lilofanya vijana wa Afrika sasa kufanya maandamano kupinga matokeo ya kile kinachoendelea hivi sasa.
Ni ijumaa ya tarehe 29 Agosti, 2025 ambapo katika makao makuu ya nchi ya Ghana kunaonekana maelfu wa watu mbalimbali wengi wao wakiwa ni vijana wenye mabango tofauti tofauti wakitaka kukomeshwa kwa ukuaji wa madeni ya nje ambayo kulingana na ripoti ya shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) deni la nje la Afrika limefikia dola trilioni moja ($1 trilioni) na deni hili limeongezeka karibu mara mbili ndani ya miaka minne hivi (kuanzia 2024 mpka 2024). Hali hii ni mbaya kwani kwa sasa deni la nje la nchi za Afrika ni karibu asilimia 60 ya pato la taifa kwa kigezo cha GDP. Athari za kukua kwa deni la taifa ni kwamba kuna sehemu kubwa ya fedha za umma zitatakiwa kua zinalipia madebni ya nje badala ya maendeleo. Wakati huo huo mikopo hiyo haikutumika moja kwa moja kwenye miradi inayoweza kua ina faida sawasawa na matarajio au ikawa fedha hizo zilifujwa kabisa kwa hio hakuna kilichofanyika. Hii ni gharama zaidi ya mara mbili kwani wakopeshaji wataendelea kukudai kulipa kwa riba ileile kubwa.
Kwa hio vijana kutoka nchi mbalimbali za Afrika wameamua kuandamana ili kudai kufutwa kwa deni la nje la Afrika lakini pia wakitaka mageuzi kwenye taasisi za fedha za kimataifa kama vile Shirika la fedha dubiani (IMF) na Benki ya Dunia (WB) na serikali wakopeshaji kufuta au kusamehe deni la Afika na kuweka mazingira rafiki kwa nchi za Afrika kufikia mikopo ya kimataifa kwa masharti nafuu tofauti na hali ilivyo hivi sasa. Nchi nyingi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara zinakabiliwa na changamoto kubwa ya ukuaji wa deni la nje huku njia za ulipaji wa madeni hayo zikiwani finyu na hivyo kuziweka katika hatari ya mdororo wa kiuchumi.
Waandamanaji wanahitaji pia viongozi wa Afrika kukaa na wakopeshaji kuja na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuweza kutatua tatizo la deni la nje na pia kufanya mageuzi katika muundo wa taasisi za fedha za kimataifa na mataifa tajiri ili kuzuia matatizo makubwa baadaye. Swala la kuhitaji mfumo mpya wa kimataifa wa uchumi lilianza kupigiwa kelele tangu 1970s lakini hakuna kilichobadilika.
Na sasa kutokana na kuendelea kuimarika kwa muungano wa BRICS+ kunaweza kutoa fursa kwa ajenda hii kupata nguvu kwa sababu tayari muungano huu umeonesha kua endapo watapambana na ubepari wa nchi za magharibi na Marekani ambazo ndio zimeshikilia uchumi wa dunia kwa sasa, kuna nafasi za kushinda. Kitu ambacho Waafrika wanakipigania hivi sasa kinaungwa mkono na Urusi, China na India. Kwa hio tofauti na miaka ya nyuma kwa sasa mazingira yanaweza kua upande wa Afrika. Ila kikwazo kikubwa kitakua ni dhamira ya viongozi wa Afrika kuleta mabadiliko ya kweli.

Comments
Post a Comment