Muendelezo wa vitisho baina ya korea kaskazini na Marekani kwa mwezi wa nne 2017.
Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC)
Makombora ambayo inasafikika yanamilikiwa na Korea Kaskazini.(Picha kwa msaada wa BBC)
April
Korea kaskazini ilirusha kombora jingine kulenga bahari ya Japan na kitendo kilichozua hofu kubwa toka Japan.
Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.
Katika Mji wa Pyongyang,Kombora lenye uzito wa kati lilirushwa upande wa mashariki mwa bandari ya Sinpo kuelekea bahari ya Japan.
Baada ya hapo Marekani iliahidi kuwalinda washirika wake dhidi ya uchokozi wa Korea kaskazini.

Marekani imeahidi kuimarisha uwezo wake wa kijeshi ili kukinga washirika wake wa mashariki mwa Asia dhidi ya Korea kaskazini.
Ikulu ya white house inasema rais Trump amemhakikishia waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kwamba Marekani itasimama pamoja na Korea kusini na Japan, katika kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.
Trump kwa mara nyingine anaionya Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.
Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Korea Kaskazini nayo yaijia juu Marekani na kuapa kulipiza kisasi kama marekani itajaribu kuishambulia.
Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia.
Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.
"tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo.
''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia''.
Korea kaskazini ilisema itatumia silaha kali kujilinda dhidi ya marekani wakati huo huo China na Marekani zilitaka mzozo wao na korea utatuliwe kwa njia ya amani japo Marekani bado ilisisitiza kua "machaguo yote yalikua mezani" ikiwemo matumizi ya jeshi.
Korea kaskazini ilifanya gwaride la nguvu la kijeshi kuadhimisha 'siku ya jua'. Gwaride hilo liliambatana na maonesho ya silaha za kivita za Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na makombora yanayosemekana kua ni mapya kabisa.
'Siku ya jua' mjini Pyongyang iliadhimishwa kwa maonyesho ya makombora, mwendo bila kukunja magoti na mapambo ya nguo (pom-poms)
Korea Kaskazini imeandaa gwaride kubwa na la kusisimua katika mji mkuu Pyongyang kuadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo, Kim Il-sung.
Maadhimisho hayo yanajulikana kama 'Day of the Sun' ama siku ya jua, kwani Kim Il-sung mara nyingi huwa anatambulishwa kwa ishara jua.
Maadhimisho hayo yalionekana kama maonyesho ya nguvu za kijeshi wakati kumekuwa na uhusiano baridi baina ya Marekani na Korea Kaskazini.
Mwandishi wa BBC aliyehudhuria maadhimisho hayo anasema kwamba alihisi ardhi ikitetemeka wakati wanajeshi walipokuwa wakipita pamoja na makombora.
Wanajeshi wanawake wakitembea bila kukunja magoti katika onyesho la kusisimua.
Bendera ya Korea Kaskazini ilipeperushwa kwa nguvu.
Kundi la wanaume wakiwa wamebeba mapambo yanayowekwa kwenye nguo ama kofia (pom-poms)
Ndege angani zimeunda umbo la takwimu 105.
Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un, mjukuu wa rais mwanzilishi wa taifa hilo, awapungia mkono watu waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mwanajeshi apiga picha za maadhimisho hayo.
Korea kaskazi ilifyatua kombora ambalo halikufanikiwa baada ya kulipuka muda mfupi baada ya kupaa.
Korea kaskazini yasisitiza kuendelea kujaribu makombora yake kila itakapobidi.
Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake, Afisa wa juu nchini humo ameiambia BBC mjini Pyongyang, ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.
''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka," alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.
Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.
Korea kaskazini imesema itaizamisha meli ya kivita ya marekani kwa 'shambulio moja'.
Korea Kaskazini iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.
Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishwa kwa shambulizi moja.
Kikosi maalum cha wanajeshi wa marekani kiliwasili Darwin, Australia kwaajili ya mazoezi ya pamoja kwenye bahari ya pasifiki.
Kundi la meli za Marekani zikiongozwa na USS Carl Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.
Kuna mengi sana yametokea lakini kwa hayo nadhani umeona jinsi kila upande unavyojigamba na hatari iliyopo ya dunia kuingia katika anguko la vita ya tatu ya dunia na itakua ni vita mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa.
Siku kadhaa zilizopita ilitoka taarifa kua rais wa Marekani Donald Trump alifanya mazungumzo ya simu na mwenzake Xi Jin Ping wa China na Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe huku China ikisisitiza kuwepo kwa amani kwenye rasi ya Korea. Mazungumzo hayo yanajiri wakati ambapo kuna taarifa kua kundi la meli za kivita toka Marekani zikiongozwa na USS Carl Vinson zitawasili rasi ya Korea muda wowote kuanzia sasa. Lakini Korea kaskazini ameendelea kushikilia msimamo wake kua uwepo wa meli hizo kua "ni kitendo cha hatari sana kinachofanywa na wale wanaotaka kuanza kwa vita vya nyuklia."
"Marekani haipaswi kukimbilia vita na inapaswa kuchukua tahadhari kwa madhara yoyote yatakayotokana na kitendo cha kijinga cha uchokozi wa kijeshi" lilinukuliwa gazeti la serikali la Rodong Sinmun. Marekani na washirika wake wanahofia kua Korea kaskazini inapanga kufanya majaribio zaidi ya makombora na zana za kinyuklia kitendo kinachoiudhi Marekani na washirika wake pamoja na China.

Mshirikishe na mwenzako habari hii.
No comments:
Post a Comment