Tuesday, 2 May 2017

MAJIGAMBO YA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI (1)

DUNIA YA VICHWA VIWILI VISIVYOTOSHANA.

Meli ya kubeba ndege na makombora ya Marekani ikiwa njiani kuelekea eneo la bahari la korea kufuatia mvutano mkali baina ya Korea na Marekani.


Kuna wasiwasi wa dunia kutumbukia kwenye vita mbaya ya nyuklia kutokana na vitisho baina ya Marekani na Korea kaskazini. Kumekuwepo na vita za maneno na vitisho baina ya Washington na Pyongyang watishiana kupigana baada ya kipindi kirefu cha bila maelewano baina yao.
8Kinachosubiriwa kwa sasa ni nani ataanza kumshambulia mwingine?!
Tangu mwaka huu uanze Korea ameshanya majaribio kadhaa ya nyuklia na kuahidi kufanya mengine kila wiki na kila wakati watakapo kua tayari. Nini tunakijua kuhusu Korea na Marekani kwa mwaka huu??
January.
ΔTrump alipuuza taarifa za Korea kua na kombora la masafa marefu.
Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.
Bwana Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.
ΔTrump alisema kua mpango wa kombora la masafa marefu la korea kaskazini usingefanikiwa lakini hakusema kivipi na Korea kaskazini ikasema italifanyia majaribio kombora hilo popote na muda wowote.
February.
ΔKorea kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu linaloweza kubeba kichwa cha silaha za nyuklia.

ΔTrump akasema kua nchi hio ni "tatizo".
Rais wa Marekani Donald Trump ameizungumzia Korea ya Kaskazini baada ya kitendo chake cha hivi karibuni cha kurusha kombora lenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia kwamba nchi hiyo ni tatizo kubwa mno.
Trump alitoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi ya Canada, Justin Trudeau katika ikulu ya Marekani, Trump amesema kwamba ataishughulikia na nchi ya akizungumza kwa msisitizo juu ya kauli hiyo.
ΔKorea kaskazini iliishutumu China kua ni kibaraka wa Marekani.
Korea kaskazini ilifyatua kombora kuelekea sehemu ya bahari ya Japan.
March
ΔChina ilimuonya Marekani kua makini na Korea kaskazini.
Wakati huo huo Korea kaskazini ilitishia kuishambulia Japan.
Na pia ilifanyia majaribio injini yake mpya ya kurushia makombora angani.
ΔVyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.
Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.
Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.
ΔMarekani ilisema haitoivumilia tena Korea kaskazini.
Sera ya Marekani ya kuwa na subira dhidi ya Korea Kaskazini imeisha, kulingana waziri wa maswala ya nje nchini humo Rex Tillerson wakati wa ziara yake nchini Korea Kusini.
''Njia zote tulizotumia ziko wazi na sasa tunatafuta njia nyengine za kidiplomasia ,usalama na kiuchumi'' ,alisema.
Kwa kipindi cha takribani miaka 20 tumekua tukiisihi Korea kuachana na mpango wa nyuklia lakini juhudi hizo zimegonga mwamba.
Kuuawa kwa ndugu wa Kim jong un aitwaye Kim jong Nam nchini Malaysia.

No comments:

Post a Comment