'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU
Katika ulimwengu wa kijasusi mambo mengi hutokea na wakati Fulani hivi ni ngumu kuamini kama hayo yanayotoka katika ulimwengu huo ni kweli au ni stori za kufikirika. Naam, ni takribani miaka 50 sasa tangu Israel ilipopata taarifa za shambulio katika ardhi yao ndani ya saa 24 kabla ya tukio kutoka kwa “ANGEL” kwa maana ya “MALAIKA”. Ambapo bila taarifa kutoka kwa huyu "the Angel" kusingekua na Israel na kama ingekuepo basi ingekua tofauti sana na iliyopo sasa.
Februari
2, 1944 wakati dunia iko katika mapambano makali kati ya udikteta wa Hitler na
demokrasia ya Magharibi ndipo ambapo “the Angel” alizaliwa kule Cairo Egypt.
Alizaliwa katika famillia yenye uwezo mzuri kiuchumi kwa hio alilelewa vizuri
sana ana wazazi wake. Alipata nafasi ya kusoma katika Chuo kikuu cha Cairo na
alihitimu katika “Chemical Engineering” mwaka 1965 akiwa na miaka 21. Akaweza
kuandikishwa jeshini mwaka huo na huko akafanikiwa kukutana na binti mrembo
sana mwenye miaka 17 akiitwa Mona Abdel Nasser binti wa pili wa Gamal Abdel
Nasser ambae alikua Rais wa Misri wakati huo.
“The
Angel” anapingwa na Gamal Abdel Nasser lakini historian a uwezo wa dogo
vinambeba anakubaliwa kumuoa binti wa Rais mwaka 1966. Anaingia kufanya kazi
ndani ya Ofisi ya Rais sasa ambaye pia ni Mkwe wake. Wakati huo huo mkwe wake
hamuamini “the Angel” (Alikua anafahamika kwa jina lake halisi ambalo tutaliona
baadae). “the Angel” akawekewa majasusi wengi wa siri na wengine walikua ni
watu waliokua wanamsimamia katika kazi kwa hio walimfuatilia katika mstari wa
utendaji kazi na hawa walijulikana.
![]() |
Rais Gamal Nasser, Mona Nasser na Ashraf Marwan |
Kati ya 1969 na 1973 “the Angel” alifanya kazi kubwa sana na Gamal Nasser alimtuma katika baadhi ya mission chache za siri sana. Alifanya kazi ya kuingiza silaha kutoka Marekani ambazo zilipaswa kupelekwa kwa vikundi vya wapiganaji wa Palestina na alizishawishi nchi za Kiarabu kutouzia Mafuta Marekani na kusababisha uhaba mkubwa mwa Mafuta na mdororo wa uchumi duniani kama malipizi ya vita vya siku sita ya mwaka 1967.
“The
Angel” anaenda London lakini anafanya kitu cha kistua kidogo. Anakamata simu
nyekundu (simu za vibandani kule London) anapiga namba za ubalozi wa Israel na
kusema anataka kuongea na mtu wa Intelijensia katika ubalozi wa Isael.
Sekretari haelewi mbona lafudhi ya Kiarabu? Ila sio kesi yeye si wa kwanza
akamuunganisha na watu wa kitengo. Anawaambia Mossad (Shirika la Ujasusi la
Israel) kwamba anataka kua jasusi wao! Kwa mtu kama “the Angel” mfanyakazi
ofisi ya Rais na Rais ni Mkwe wake ilikuaje? Inasemekana alipishana na mkwe
wake juu ya mipango ya kuivamia Israel na mkwe wake alimpigia goti binti yake
kwamba atalikiane na “the Angel” kwani alikua na dili chafu na mtu wa kamari.
Kwa hio alitaka kumuonesha mkwe wake kua alikua na uwezo mkubwa ila hadi
kuhatarisha usalama wa taifa lake?
![]() |
The 'Angel' |
Mwaka
1970, Gamal Abdel Nasser anakufa na nafasi yake inachukuliwa na Anwar El
Sadaat. Anafanya mabadiliko maubwa sana lakini lengo la kuivamia Israel likawa
pale pale. Na sasa mipango ya Misri juu ya Israel inawafikia moja kwa moja
Israel lakini bado Mossad hawakumuamini sana. “the Angel” aliwalisha MOSSAD
taarifa za uongo mara mbili kati ya May na Oktoba 1973. Hapa Mossad wakawa
wanatilia mashaka taarifa zake lakini saa 24 kabla ya tar 6 oktoba 1973, “the
Angel” alituma ujumbe wa siri kua alitaji kuongea na boss wa Mossad moja kwa
moja ni dharura mno.
Issue ilikua hivi kwanza tar 4/10/1973, "the Angel" anamtumia mwanamke mmoja hivi ili afikishe ujumbe kupitia "dead phone" (huwezi kui track) kwenda Mossad na akasema the Angel anahitaji kuonana na "general" top boss wa Mossad wa kuitwa Zvir Zamir siku ya pili yaani tar 5/10/1973 kujadiliana juu ya "kemikali". Hilo neno likawastua sana Mossad taarifa ikafika kwa Boss (Zamir) na akaogopa kuna nini? The Angel lazima anakitu nyeti sana. Akakwea kindege mpka London na anapewa taarifa ambayo dah.... anainua simu kumpigia mkuu wa Majeshi ya IDF wakati huo sikukuu ishaanza.
Taarifa ikifika kwa
bibi mmoja hivi ambaye wakati wewe unavuta oksjeni ili uishi yeye alikua
akivuta sigara na huyu anafahamika kama “the Iron Lady of Israel” au kwa majina
yake ya Golda Meir waziri mkuu wa kwanza na wa pekee mwanamke nchi Israel. Anapokea
taarifa anatetemeka haamini anachoambiwa basi waziri wa ulinzi mzee wa jicho
moja Moshe Dayan nae anaskia haelewi na ahujui inakuaje. Taarifa za hio vita Israel
walikua wanapata kutoka kwa majasusi wengine pia ila iliyokuja kutoka kwa “the
Angel” ilikua ya moto mno na iliwafikia viongozi wakuu bila kubadilishhwa
chochote ili wafanye maamuzi bila makosa.
Taarifa
inasema 'Israel inavmiwa kesho...' Misri na Syria zimepanga mashambulizi ya kushtukiza na yanaanza kesho majira ya saa 12:00 jioni na (lakini kumbe muda ulibadilishwa siku ya tar 6/10/ 1973 mashambulizi yalianza saa 8:05 mchana). Wakati huo wanajeshi na watu wote wako katika mapumziko ya sikukuu ya kiyahudi
inayohamika kama Yom Kippur. Wanajeshi ambao wako active hawezi fanya chochote
kile. Golda Meir anasema tunahitaji kukusanya jeshi (mobilization) wengine
wakasema ni hatari tutapigwa hata kabla ya kesho. Anauliza tunaweza kupata
wanajeshi wangapi anaambiwa 22,000 anachoka anasema nataka wanajeshi 120,000
watu wanaruka juu haiwezekani anasema tofauti ni nini 22,000 au 120,000
anaondoka anamwambia waziri wake wa uliunzi jeshi liwe na watu 120,000 (wa
kuanzia tu).
Taarifa
ya “the Angel” iliwasaidia sana Israel kupanga kwa haraka mpango wa vita na
kujua silaha ambazo Misri na Syria watazitumia. Bila hii taairfa basi Historia
ya Israel leo ingekua tofauti sana. The Angel alilipwa $100,000 (zaidi ya TZS
240,000,000). Hata hivyo vita vya mwaka 1973 ndio vira pekee tangu 1948 mpka
sasa ambapo wanajeshi wengi wa Israel walikufa na uharibifu mkubwa kufanyika
Israel. Wanajeshi zaidi ya 2800 walipoteza maisha. Inabakia kama vita mbaya
zaidi kwa Israel. Tukio kama like la 6/10/1973 limetokea tarehe 7/10/2023.
Nadhani Israel wanamkumbuka sana “the Angel” NA KATIKA KUADHIMISHA HILO MOSSAD
walichapisha picha ya “the Angel” akiwa na kachero mwingine (handler) wa Mossad
enzi za uhai wake.
![]() |
Picha hii ilichapiswa na Mossad 2023 ambapo Ashraf Marwan alikua yuko na 'handler" wake wa Mossad |
UTAMBULISHO HALISI
“The
Angel” ilikua ni code ambayo Mossad waliitumia juu ya Ashraf Marwan ambaye
alifanya kazi nao kuanzia 1970s-1998. Na utambulisho wake haujawahi kufichuliwa
mpka mwaka 2002. Kwa hio kila mtu alitamani sana kumjua the Angel alikua ni
nani lakini haikua rahisi hadi mwaka 2002 ambapo mwana taaluma wa Israel Ahron Bregman aliweza kufichua utambulisho wake katika mahojiano na jgazeti la kila siku la Misri la Al Ahram. Mossad wanasema huyu ndie alikua
akitoa taarifa zenye tija kubwa zaidi za Misri kwa Israel. Taarifa zake
waliziamini sana isipokua zile mbili za mwanzo mwaka 1973.
Lakini
msimamo huo wa Mossad ulipata upinzani mkali kutioka kwa mfichuzi wa
utambulisho wa bwana Ashraf Marwan amabae anasema Marwan alifanya kazi kama
“Double Agent” wa Misri na Israel na kwamba jamaa alikua akiilisha Mossad
taarifa za uongo tangu awali kwa hio ailikua anaisaidia Egypt. Huenda jamaa ana
hoja anasema hata zile taarifa mbili za mwanzo zilikua ni kuichanganya Mossad
isijue ukweli wa kinachopangwa na Misri.
Hili
huenda lina ukweli kiasi lakini ikiwa ndivyo kwanini aliwaambia mpango mzima wa
vita wa oktoba 6 1973 ambao kwa sehemu kubwa zaidi uliiharibu Misri na kuiokoa
Israel na dhahma? Na hoja ya kwanini ndani ya saa 24? Inasemekana Sadaat
albadili ghafla mpango wa vita wakati Marwan amekwenda London. CIA pia nao
hawaamini kama Marwan alikua ni double agent wanaamini kazi yake iliisaidia
sana Israel kuliko Misri. kutoka kwa kwa Ahron Bregman tunakuja mpka 2016 ambapo tunakutana na mwandishi nguli na Profesa wa kuitwa Bar-Joseph Uri alieandika kitabu kinaitwa The Angel: The Egytptian spy Who Saved Israel nae anasema Ashraf Marwan hakua double agent ila alifanya kazi kwa upande mmoja wa Mossad tu. kitabu hiki kimeumika kutengeneza filam ya Netlix kwa jina hilo hilo.
Ashraf
Marwan alikutwa amekufa mwaka 2007 nyumbani kwake London kwa kuanguka kwenye
Balcony ya nyumba yake. Kifo chake kinabakia kitendaawili ndani ya ulimwengu wa
kijasusi kwa sababu kifo cha aina ile kiliwapata pia Maafisa wastafu wa Ujasusi
wa Misiri ambao labda Mossad iliwaona walishiriki kuitesa Israel. Mona na
mwanae wa kwanza pia wanaamini Marwan aliuliwa na Mossad. lakini kuna mtu mmoja anajutia sana nae si mwingine ni Aichua utambulisho wake kwani alikufa muda mfupi baada ya kupanga kukutana nae huko london sasa nani muhusika? bado ni fumbo.
Na
cha kushangaza baada ya kifo chake, Ashraf Marwan aliweza kuzikwa kama shujaa
huko Misri na Hosni Mubarak ambae alikua rais wa Misri kwa wakati huo alisema
kua Ashraf Marwan alikua ni shujaa kwa nchi yake ya Misri kwa kazi kubwa
aliyoifanya hata hivyo sio muda wake au muda bado wa kuyajua yale ambayo Ashraf
Marwan aliyafanya.
Hadi
hapo tutakapokua na uwezo kuyajua hayo basi itoshe kusema, Ashraf Marwan alikua
ni zaidi ya Jasusi na itachukua muda mrefu labda kupatikana tena Jasusi wa
uwezo wake.
“THE
ANGEL”
MOSSAD
NA UJASUSI WA DUNIA
NETANYAHU
ATAVAA VIATU VYA GOLDA MEIR?
No comments:
Post a Comment