![]() |
Moshi mkubwa baada ya kombora kupiga sehemu ya majengoya Gaza |
Ni
zaidi ya miezi miwili tangu Oktoba 7 ambapo wanamgambo wa HAMAS waliweza
kuvamia kusini mwa Israel na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu na
kibinadamu na kugharimu maisha ya zaidi ya Waisrael 1200 huku wengine zaidi ya
240 wakichukuliwa mateka mpaka ukingo wa Gaza.
Benjamin Netanyahu a.k.a Bibi awali alivikosoa vikosi vya jeshi la Israel kwa kushindwa kuzuia shambulio hiilo baya ana la aibu kwa Israel lakini baadae aliomba radhi na ujumbe wake huko X (zamani Twitter) ukaondolewa. Netanyahu aliapa kwamba Israel italipa kisasi juu ya tukio hilo na kwamba Hamas watalipa gharama kubwa na kwamba ni lazima kundi la HAMAS liangamizwe kabisa. Je kauli yake inawezekana? Umeskia nini kuhu Isarel? Inalindwa lakini unajua nini kuhusu HAMAS? Ni kikundi cha magaidi au ni zaidi ya hapo? Fuatilia kwa makini…
Ili
kuangamiza kundi hilo la Hamas, tar 09/10/2023 Israel ilianza mashambulizi ya
anga usiku na mchana upande wa Kaskazini wakilenga katika miundombinu na kambi
za Hamas na pia iliweka vizuizi vya kuingia na kutoka Gaza. Hakuna kuingia wala
kutoka chochote. Waliharibu chochote kilichohusiana na HAMAS na kuandaa
mazingira kwaajili ya uvamizi wa ardhini.
Tar
27 Oktoba, Israel ikavamia Gaza kupitia vikosi vyake vya ardhini. Hadi wakati
huo hospitali za Gaza zilikua zimezidiwa na 50% ya majengo yote ya Gaza yalikua
yamebomolewa kwa makombora mazito ya Bunker Boosters ya Israel. Mapigano makali
kati ya IDF (Israel Defensive Force) na Hamas yalipamba moto huku upatikatanaji
wa taarifa ukiwa mgumu. Umoja wa Mataifa ulitoa tahadhari ya hali ya kibinadamu
Gaza na kutoa wito wa kusitisha mapigano lakini Marekani, Israel na washirika
wao walisema hakuna kusitisha mapigano mpaka HANAS iangamizwe.
Hadi
sasa zaidi ya Wapalestina 18,205 wakiwemo wanamgambo wa Hamas wameuwa huko Gaza
na zaidi ya wanajeshi 100 wa Israel wameuwa na kupekea vifo vya jumla kwa
Israel kua zaidi ya 1400. Kuzingatia uharibifu na kuzorota kwa hali ya
kibinadamu kila mtu anasema ‘inatosha sasa” lakini Israel ya Benjamin Netanyahu
a.k.a Bibi anasema bado ni Mpaka HAMAS isambaratishwe. Hili linaungwa mkono na
Marekani lakini Marekani inaona bado Israel haifanyi vya kutosha kupunguza vifo
vya raia kwani mpaka sasa IDF wanasema kwenye kila watu watatu wanaokufa kuna
mwanamgambo mmoja wa Hamas. Kwa hio wanamgambo wa Hamas waliokufa ni zaidi ya
5000. Na kwa mara ya kwanza wiki rais wa Marekani anasema Israel inaanza
kupoteza ‘sapoti’ na akasema Netanyahu na serikali yake wanapaswa kubadilika.
Israel
imeshashinda vita hivi LAKINI BADO HAIWEZI KUHESABIA IMESHINDA ENDAPO
haitawakamata na au kuwaua viongozi wakuu au mashuhuri wa Hamas. Huenda kutowafikia
hawa ndio maana Israel haitaki kuhesabu kwamba vita Gaza imeisha. Kwa maoni
yangu Hamas ni zaidi ya kikundi cha wanamgambo; Hamas ni itikati na ni wazo
lililofungamanishwa na dini kwa hio kuliondoa itakua vigumu ila tawi la kijeshi
la Hamas hilo sina shaka kwamba Israel wanafaulu. (soma makala zilizopita juu
ya HAMAS).
Watu pasua kichwa wanaomnyima usingizi Benjamin Netanyahu pamoja na IDF ni watu ambao Israel kwa wakati mmoja walikua na nafasi ya kuwamaliza lakini waliwaponyoka na sasa ni kama mkuki moyoni. Ni hadi wapatikane hai au wakiwa wafu ndio mambo ya Gaza yatakua yameisha
Yahya Sinwar
huyu ni nambari moja katika orodha ya "the most wanted". Muumini wa Suni na wazazi wake walifurushwa huko Ashkelon katika vita vya 1948 na kukimbilia huko kusini mwa Gaza. Alizaliwa 1962 katika kambi ya wakimbizi huko Khan Yunis. Akashiriki katika harakati za waarabu na alikamatwa na Israel 1988 baada ya kuwaua na kuwateka Wayahudi kadhaa. Akahukumiwa jela maisha. Akiwa Gerezani alisoma sana vitabu juu ya Waisrael ili kua na uelewa juu ya “adui’ na alijifunze Kiebrania. Madaktari wa Israel waliyaokoa maisha yake baada ya kuondoa kitu kama uvinbe karibu na ubongo wake lakini fadhila alizolizipa ni zile za Oktoba 07.
2011
aliachiwa huru kupitia mpango wa kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hamas
yeye pamoja na zaidi ya Wapalestina 1000 ambapo Hamas walikua wakimshikilia
mwanajeshi mmoja wa Israel kwa jina Gilat Halit. 2017 akashikilia uongozi wa
juu kabisa wa Hamas na hapo mapigano na Israel yakazuka upya 2018, 2020, 2022
na 2023 na huyu inasemekana ndio ‘masterminder’ wa mashambulizi ya Oktoba 07. Umeshajua
kwanini IDF hawawezi kulala kama hawampati Yahya Sinwar ni mtu hatari mno.
Mohamed Deif (Paka mwenye roho 9)
Mtu
hatari sana ambae aliwekwa katika “the most wanted” ya Israel mwaka 1995. Inasemekana
ukisema Gaza wana mtandao wa mahandaki basi mwamba huyu ndie aliye nyuma ya
kazi hio. Na amekua kiongozi wa tawi la kijeshi la Hamas Al Qassam Brigades
tangu 2002 hadi sasa. Alikamatwa na Israe mwaka 2000 lakini alifanikiwa
kutoroka na hakuna taarifa zake hata picha tu kupata ni ngumu. Inasemekana amekwepa
zaidi ya majaribio 7 ya kumuua japo kuna baadhi ya sehemu ya viungo kama mkono,
jicho na mguu huenda akawa hana au viliwahi kuathiriwa. Huyu pia IDF wanasema
ana uwezo mkubwa sana wa kuidhuru Israel kwa hio ni lazima auwawe.
Marwan Issa
Alizaliwa
katika kambi ya wakimbizi huko Palestina na mengi hayafahamiki sana wakati wa
utoto wake lakini inasemekana aliwahi kua miongoni mwa wanachama wa Muslim
Brotherhood ambalo baadae HAMAS ilizaliwa. Huyu ni kamanda msaidizi wa Al
Qassam brigades ambalo ndio tawi la kijeshi la Hamas.
![]() |
Marwan |
Hawa
ni watu muhimu wanaofadhili kundi zima la Hamas lakini hawako Gaza hawa
wanaishi maisha ya Kifahari sana huko Qatar. Hawa ndio viongozi wa ngazi za juu
zaidi wa tawi la kisiasa la HAMAS ambao huratibu na kufadhili kundi hilo.
Ismail Haniyeh ndio top wa Hamas baada ya kuachiwa kiti hicho na Khaled Mashaal
mwaka 2017 na kumbuka 2006 alishawahi kua kiongozi wa Palestinian Liberation
Organization (PLO) lakini aliondolewa madarakani mwaka mmoja tu baadae kutokana
na HAMAS kujaribu kumuondoa kinguvu Mahamoud Abbas ambaye kwa sasa ndiye
kiongozi wa PLO.
Uwepo
wa hawa watu bado utazidi kua tishio kwa Israel na utafutilia mbali ndoto za
Netanyahu za kuweza kuiangamiza HAMAS milele. OSAMA Bin LADEN aliwanyima
Marekani usingizi hadi Barack Obama alipomaliza kazi 2012 na sasa hawa viongozi
wa HAMAS wanainyima usingizi viongozi wa Israel na ni lazima waweze kuondolewa.
Hili liko wazi na ndio maana Bibi (Netanyahu)
akamuagiza mkuu wa IDF kua ahakikishe anatafuta na kuta vichwa viongozi wa
Hamas na kamanda akamwambia hilo halina shaka ‘Hamas leader lives in borrowed
time” kwamba “viongozi wa Hamas wanaishi katika muda wa kuazima” ni swala la
muda tu kabla hawachauawa.
Tamko
lolote la ushindi dhidi ya Hamas, kwa maoni yangu litahusisha kukamatwa na au
kuuwa kwa viongozi hao na wengine wa ngazi za juu za Hamas. Kwa kua Israel
inataka kuona Gaza isiyokua na HAMAS na hili linawezekana kwa viongozi wao wa
ngazi za juu kuuawa. Viongozi wa ngazi za juu zaidi wa HAMAS wamekua wakiishi
Qatar lakini kwa taarifa za hivi karibuni ni kwamba viongozi hao wanahofia
maisha yao kwani Mossad wako kazini na inasemekana wamekimbia Qatar kukwepa
vichwa vyao kutenganishwa na kiwiliwili.
Gharama ya vita katika ukingo wa Magharibi ni kubwa mno na hivyo ni wakati wa jumuia ya kimataifa hasa Umoja wa mataifa kuona namna sahihi ya kumaliza mgogoro huu kupitia mazungumzo kwani pande zote mbili zinazohasimiana haziko tayari kwa mazungumzo. Kama jamii ya karne ya 21 tunapaswa kuona kwamba sasa inatosha kwa Hamas kuacha uchokozi na kwa Israel kuacha mashambulizi lakini pia kuwe na kubadilishana mateka kwa pande zote mbili.
Maoni,
maswali na ushauri basi usisite kutuandikia kupitia njia zifuatazo;
Email:
karlrck@gmail.com
Simu:
0787 505 800
WhatsApp:
0629293768
No comments:
Post a Comment