Suala la ulinzi na usalama ni moja ya mambo makubwa na muhimu ambayo kwa kipindi kirefu yamekua yakisumbua vichwa vya watunga sera na viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali makubwa duniani. kufuatia vitisho vya vya uliokua muungano wa Soviet ulipelekea kuundwa kwa Umoja wa kujihami wa NATO mwaka 1949 na baadae muungano wa Soviet uliunda umoja wake wa Warsaw Pact mwaka 1955.
Tangu hapo Marekani imekua taifa ambalo hujachangia kiwango kikubwa cha bajeti kwaajili ya NATO huku mataifa mengine yakichangia kidogo. Hii inatokana na muundo wa NATO na malengo yake wakati inaundwa. Lakini tangu kuchaguliwa kwa Donald Trump kama rais mpya wa Marekani mwaka 2016 amekua mkosoaji mkubwa wa NATO na kuyataka mataifa ya Ulaya kuchangia zaidi au Marekani haitachangia.
Msimamo wa Donald Trump ndio umewasukuma viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya kuja na Mpango wao wa kuunda ndege zao za kivita (European Fighter Jet) ambazo ni za kizazi kijacho. Makubaliano hayo ymefikiwa na mawaziri wa ulinzi wa Ujerumani, Ufaransa na Uhispania. Mfumo huo wa kujilinda wa anga (The Future Combat System) utakua tayari unatumika ulaya mwaka 2040.
Mpango huu ambao gharama zake rasmi bado hazijawekwa wazi utatimiza mahitaji ya ulinzi wa anga wa mataifa ya Ulaya kwa wakati huo. serikali za Ufaransa na Ujerumani zimepanga kuwekeza hadi dola 4.5billion ($ 4.5bn) hadi mwaka 2025. Licha ya kua wapinzani wanaukosoa mpango huu,
swali la msingi ni je mataifa ya Ulaya yanatafuta njia mbadala? Ikumbukwe pia mataifa ya Ulaya yamewekeza katika ndege za F-35 zinazozalishwa nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment