Sunday, 14 May 2017

KOREA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA JIPYA.

Google
Uwezo wa makombora yanayomilikiwa na Korea kaskazini. 

Korea kaskazini imerusha kombora jingine mapema leo jumapili ambalo liliruka karibu 700km, hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Korea kusini. Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tu tangu rais mpya wa Korea kusini kushika wadhifa wa urais hapo jumatano. Rais mpya wa Korea alisisitiza kua yuko tayari kufanya mazungumzo na utawala wa Pyongyang kama mazingira yataruhusu.

Kombora hilo la leo mapema lilifyatuliwa kwenye eneo la Kusong, kaskazini magharibi mwa Pyongyang ambapo mwezi februari pia Korea kaskazini ilifanikiwa kufyatua kombora la masafa ya kati.
Machache kuhusu kombora la leo jumapili.
    •Limeruka zaidi ya 700km na kufikia kima cha zaidi ya 2000km na lilikua likiruka kuelekea juu. (projectile) na lilitua kwenye pwani ya mashariki mwa Korea na Japan.
Ni aina mpya ya kombora kutoka korea kaskazini. Mpaka sasa Pentagon wanasema wanafanyia kazi taarifa walizonazo kuweza kubaini ni kombora la aina gani.
Kama lingerushwa kwa viwango vya kawaida huenda lingesafiri kiasi cha 4000km au zaidi. Kwa uwezo huu inamaana kambi za kijeshi za Guam za Marekani zinaweza kupigwa kwa makombora kutoka Pyongyang. 
Ni kombora la kwanza kufanikiwa baada ya kufeli kwa majaribio manne mfululizo kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita. 
Limeruka kwa takribani dakika thelathini hivi.
China inazitaka pande hasimu na Korea kaskazini kujizuia na upande wowote usifanye chochote kitakacho chochea mzozo huo kufuatia jaribio hilo la leo. Waziri wa mambo ya nje wa China amesema China inapingana na ufyatuaji wa makombora unaofanywa na Korea kaskazini kwa kua ni kinyume na maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa linalopiga marufuku Korea kaskazini kufanya majaribio ya aina yoyote ya makombora. "kwa muda huu hali juu ya rasi ni ngumu na tete, pande zote zinazohusika zinapaswa kujizuia na kutokufanya chochote kuchochea zaidi mvutano kwenye ukanda huu". Ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya China.
Kombora hilo lilifika umbali wa kima cha 2000km na lilisafiri kwa muda wa dakika 30 kabla ya kuanguka kati ya pwani ya mashariki ya korea kaskazini na Japan.
Kamanda wa Marekani anayeshughulika na eneo la Pacific alisema walikua wanatambua kujua aina ya kombora lakini "halikua likifanana na kombora la masafa ya marefu"(intercontinental ballistic missile-ICBM).
Nae rais wa Korea kusini Moon Jae-in aliitisha kikao cha dharura cha baraza la usalama la taifa ili kujadili hali hiyo. "Rais amesema wakati korea inabaki wazi juu ya uwezekano wa mazungumzo na Korea Kaskazini, inawezekana pale tu Korea kaskazini itakapo enesha mabadiliko ya mtazamo", alisema Yoon Young-chan mkurugenzi wa habari wa rais Moon.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amawaambia waandishi wa habari leo jumapili kua kujirudia kwa ufyatuaji wa makombora unaofanywa na Korea kaskazini ni "kaburi la vitisho kwa nchi yetu na ukiukaji wa wazi wa azimio la umoja wa maitaifa(UN).
Watu wakitazama kombora lililofyatuliwa na korea kaskazini mapema leo jijin Seoul, Korea Kusini. 

MAJIBU KUTOKA IKULU YA WHITE HOUSE_MAREKANI.
Ikulu ya marekani imejibu juu ya kombora la Korea kaskazini kua utawala huo umekua ni "tishio hatari kwa muda mrefu sana." Taarifa iliongeza kua rais Trump "hawezi kufikiri kua Urusi inapendezwa" na jaribio la hivi mapema la Korea kaskazini kwa sababu kombora hilo limetua karibu na ardhi ya Urusi kuliko Japan.
Ikulu ya Marekani pia imesema kua Marekani itaendelea kujizatiti bila woga kusimama na washirika wake ili kukabiliana na vitisho vyovyote kutoka Korea kaskazini na imeongeza kua "uchokozi" huu wa hivi punde iwe ni wito kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kua Korea kaskazini imefanya jaribio la kombora majira ya 10:30am kwa saa za Hawaii. Hili linakua ni jaribio la kwanza kufaulu kufuatia kufeli kwa majaribio mengine manne mfulululizo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Baadhi ya makombora yanayomilikiwa na Korea kaskazini. 



No comments:

Post a Comment