Picha hii ilipigwa na kituo cha televisheni cha Al jazeera japo haifahamiki ilikua ni lini.
Mtoto wa Osama bin laden anasemekana kua anapanga kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi juu ya kifo cha baba yake kilichotokea May 2013. Mtoto huyo pia (Hamza) anajiandaa kua kiongozi mpya wa kundi la Al Qaeda.
Barua binafsi aliyoiandika na kukutwa wakati wa shambulizi lililomuua baba yake inaeleza kua ipo siku moja atakuja kulipa kisasi, alisema Ali Soufan, ofisa wa zamani wa FBI alipohojiwa na kituo cha habari cha CBS News cha nchini Marekani.
"Anasema kwamba....anakumbuka 'kila jicho...kila tabasamu ulolilonipa, kila neno uliloniambia,"' anasema Soufan pia kumhusu mtoto wa Bin Laden. Soufan aliiambia CBS News kua Hamza aliandika kua anajiona mwenyewe kua kama "chuma". Soufan anasema njia ya Hamza kua kiongozi mkuu wa kundi hilo la kigaidi ilianza miaka kadhaa iliyopita wakati alipokua akitumia njia za propaganda kwenye kanda za video za baba yake Osama Bin Laden. Wakati flani alionekana ameshika bunduki na alianza kuongea kama baba yske, alisema ofisa huyo wa zamani wa FBI. "Ujumbe wake uliotoka hivi karibuni, alitoa matamshi ambayo ni sawa na baba yake, akitumia sentensi, misamiati ambayo ilitumiwa na Osama Bin Laden".
Hamza inaaminika kua ana umri wa miaka 28 kwa sasa na ameanishwa kama gaidi na Marekani. Hamza amerekodi jumbe nne za sauti kwa miaka miwili akiilenga Marekani. "Amekua akisema 'watu wa Marekani tunakuja na mtatutambua...tunakuja kulipiza kisasi kwa kile mlichomfanyia baba yangu, Iraq, Afganistani.' kila kitu kilikua ni juu ya kulipa kisasi", alisema Soufan.
No comments:
Post a Comment