Saturday, 20 May 2017
WATU WALIOKATALIWA KUISHI NCHI KAVU.
Wabajui huishi na familia zao kwenye vibanda vyao vya miti vilivyojengwa baharini kwani wamezuiwa kuishi nchi kavu na pia pia wakikaa sana nchi kavu wanajihisi kuumwa.
Dunia ina mambo mengi sana, mengine yanastaajabisha, mengine kuudhi na mengine kufurahisha. Ila hili sijui linaleta picha gani.
Bahari ni makazi ya karibu nusu ya viumbe hai waishio duniani ila sisi binadamu sio mojawapo ya viumbe hivyo kwani hatuwezi kukaa ndani ya maji ya chumvi kwa muda mrefu, hatuwezi kuzama na kukaa kwenye kina cha bahari kwa muda mrefu lakini kinyume na haya yote kuna baadhi ya binadamu karibia maisha yao yote ni baharini! Wamejenga "vijumba/vibanda" vyao vya miti huko na asilimia zaidi ya 90 wanaishi huko na sio nchi kavu! Naam, ni watu jamii ya
"WABAJAU" wanaopatikana eneo la kusini mwa bara la Asia hasa kwenye visiwa vya nchi za Ufilipino, Malaysia na Burma. Nchini Malaysia watu hawa(wakimbizi) hawaruhusiwi kuishi nchi kavu kwa hio maisha yao wanayaendeshea baharini. Wanaishi kwa kuvua samaki na kuziuza ili waweze kupata mahitaji mengine muhimu kama maji ya kunywa, mchele n.k. Watoto wao hawajui kuhusu shule, maana wakifikia umri wa miaka minne tu tayari hufundishwa namna ya kuogelea na kukamata sanaki. Wabajau wana uwezo wa kwenda chini ya bahari kwa zaidi ya meta 20 kukamata samaki.
Wakiwa pamoja na familia zao wanaishi kwenye vijumba vya miti mbali kidogo na nchi kavu.
Kuna mwandishi mmoja anaitwa Ng Choo Kia aliungana na Wabajau kwenye mtumbwi wao uliotengenezwa kwa gogo moja la mti na kutengeneza 'documentary' ya maisha yao kupitia picha.
Mkazi mmoja (43) kutoka Penang Malaysia anasema "Wabaju ni wakimbizi kutoka Ufilipino ambao kwa sasa wamechagua kuishi maisha yao yote baharini. Wanatembelea nchi kavu mara chahe ili kuuza samaki kwa ajili ya mchele, maji na vyakula vingine muhimu.
Watoto wa wabajau wote ni wabobezi wa kukamata samaki na pweza kwani uvuvi ndio chanzo chao kikuu cha maoato...watoto hawana nafasi ya kwenda shule kwa hio hakuna maisha bora ya baadae kwao."
Wakiwa wakimbizi, Wabajau hawaruhusiwi kuishi nchi kavu. Nchini Malaysia jamii hii imezuiliwa kuishi nchi kavu.
Mchana wanashinda wanazunguka majini wakivua samaki baadae kuja ufukweni kuzungukazunguka wakitafuta wa kubadilishana samaki na chakula, na hurejea kwenye vibanda vyao vya miti kabla ya jua kuzama.
Choo Kia anasema "Wakati watu wanaziona picha hizi wanavutiwa na mandhari na maisha ya kipekee ya watu hawa wanavoishi.
"Japokua, kwa maoni yangu hii ni hali inayopaswa kudhibitiwa. Watoto wanapaswa kuelimishwa juu ya elimu ya mazingira na usafi, na binafsi singelipenda watu wakulie pale."
Watoto wa jamii ya Wabajau hawana nafasi ya kupata elimu.
Licha ya maisha yao kuonekana kama ni mateso kwao lakini watoto wa jamii ya Wabajau hupata muda wa kucheza na kufurahi.
Watoto huzaliwa na kukua majini. Maisha na hatma zao ziko majini kwani wanaishi pale maji yanapokuwapo.
Mtoto huanza kuvua akifikia umri wa miaka minne tu.
Usisahau ku share habari hii na pia waweza kuacha ujumbe hapa au kwenye ukurasa wa Facebook.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment