Sunday, 19 November 2017

MUGABE ATIMULIWA UENYEKITI WA ZANU-PF



Chama tawala cha ZANU-PF cha  nchini Zimbabwe kimeridhia kumuondoa Robert Mugabe kama mwenyekiti wake na kumteua aliyekua makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa kua mwenyekiti mpya wa chama hicho.  Mnangagwa alifutwa kazi na rais Mugabe siku chache zilizopita na kutaka kumtangaza Grace Mugabe kua makamu wa rais na hatimaye aje kua mwenyekiti na baadae rais wa Zimbabwe kitu kilichoamsha hasira na sintofahamu miongoni mwa wazimbabwe wengi.

Hatua hio ilimlazimu generali wa jeshi la zimbabwe (ZDF) Gen Constantino Chiwenga kutangaza kuingilia kati mzozo huo siku ya jumatatu na siku ya jumatano  vikosi vya jeshi kulazimika kuchukua udhibiti wa serikali kwa kumuweka kizuizini rais Mugabe na kutaka atangaze kuachia madaraka hatua iliyosimamiwa na kanisa katoliki lakini taarifa zilidai kua Mugabe alikataa kufanya hivyo na pia vilizingira kituo cha habari cha ZBC.

Hata hivyo leo chama hicho tawala kimeamua kumvua uongozi mwenyekiti wake Robert Mugabe 93, pamoja na mkewe Grace Mugabe ambaye ametimuliwa kabisa ndani ya ZANU-PF.  Msafara wa magari ya rais ulionekana ukipita barabarani ukitokea kwenye nyumba la Mugabe japo haikuthibitika mara moja kama rais Mugabe alikuwapo ndani kwenye msafara huo.


No comments:

Post a Comment