Wakati dunia ikifurahia na kusherehekea mafanikio mengi na hatua kubwa iliyofikiwa na binadamu, hii sio habari na sio furaha ya kila mtu. Ni wakati ambao baadhi ya jamii zinataabika kwa mabalaa ya umaskini uliokithiri, njaa kali, majanga ya asili na vita vya wenyewe kwa yenyewe na kubwa zaidi ni SULUBU YA UTUMWA!
inaweza kua ni vigumu kuamini lakini ndio ukweli ulivyo. Vyombo mbalimbali ya habari vimeripoti uwepo wa soko kubwa la WATUMWA nchi Libya ambapo binadamu wanauzwa kama bidhaa nyingine sokoni. Wengi wa watu hao ni raia waliokimbia matatizo kama njaa, vita na umaskini kutoka nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara.
Ni ajabu na ni aibu kuona mambo haya yaliyotokea kuanzia karne ya 15 mpka 19 yameanza kujirudia tena karne ya 21 ambapo ustaarabu umeongezeka kwa kila jamii. Na hii ni njia ya kuonesha kwamba ni kwa jinsi gani mifumo yetu ya maisha ilivyo na athari kwa ustawi wa jamii yetu. Utumwa ni swala linalopaswa kupingwa vikali na jumuiya nzima ya kimataifa, watu wa dini zote na rangi zote na hali zote..! Inaumiza kuona kuna nguvu ndogo ya kukemea jambo hili.
Mashuhuda na waliopona kadhia hiyo wamethibitisha kuwepo kwa soko hilo dhalimu la utumwa nchini Libya na kuomba juhudi zaidi zifanyike kuwaokoa wengine. Mmoja wa maafisa wa Umoja wa Mataifa kitengo cha dharura alinukuliwa akisema "Kwa kadri IOM inavyojihusisha zaidi na Libya ndivyo wanavyojifunza kua ni hadithi ya machozi kwa wakimbizi wote".
Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa BBC inadai kua bei ya mtumwa mmoja ni kati ya dola za marekani 300-400 kulingana na hali ya mtu mwenyewe. Inasemekana kua wale ambao wana vipaji kama kupaka rangi, uchoraji n.k hua na bei ya juu ukilinganisha na wengine wanaosalia bila vipaji.
Libya ni lango la wakimbizi wengi kutoka enro la magharibi mwa Afrika wanaotaka kwenda Ulaya kujaribu maisha huko. Lakini wito wangu kwa vijana wa kiafrika ni kua Haijalishi nchini kwako kuna nini au nani, usipange kukimbilia Ulaya ukawe mtumwa kule. Angalia namna bora ya kupambana ukiwa hapa hapa Afrika kuliko kuwakimbia wenzako wenye fikra za kukipinga kile unachokikimbia. Utaenda huko ambako thamani yako wewe haijulikani, utafanywa chochote watachojiskia kukufanyia na hutoweza kuwazuia.
Ila kwa jumuiya ya kimataifa ninachoweza kusema ni kua hatuna muda wa kupoteza wala uso wa kuuficha, kilichobakia hapa ni kukabiliana na swala hili kule Libya ni aibu kuona kuna mwamko mdogo juu ya hili.
MIMI NAPINGA UTUMWA KWA NGUVU ZANGU ZOTE WEWE JE??!!
TAFADHARI SHARE NA WENGINE TAARIFA HII.
No comments:
Post a Comment