Monday, 20 November 2017
SAWA, HATIMAE MUGABE AKUBALI KUJIUZULU.
Kwa mujibu wa taarifa ya CNN imeripoti kua chanzo rasmi kinachofuatilia mazungumzo kati ya rais Mugabe na maafisa wa jeshi kimedokeza kua rais Mugabe amekubali kujiuzulu kufuatia hatua ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo kumuweka kizuizini kwa siku kadhaa. Hatua hii inakuja kufuatia hatua yake ya jana jumapili ambapo kwa mara ya kwanza tangu awekwe kizuizini nyumbani kwake alilihutubia taifa kupitia shirika la utangazaji la nchi hio ZBC.
katika hotuba hiyo ambayo Mugabe alitumia kuelezea hali ya kisiasa na kiuchumi nchini humo na kuonesha muelekeo mpya wa taifa hilo lakini tofauti na matarajio ya wengi waliotegemea kua angeweza kujiuzulu kufuatia kuvuliwa nafasi yake ya uenyekiti wa chama cha ZANU PF. Chanzo hicho kilidokeza kua rais Mugabe na maafisa wa jeshi walikubalina na matakwa ya Mugabe ikiwa ni pamoja na kinga ya kutoshtakiwa pindi atakapo jiuzulu na ulinzi wa mali zake binafsi za kwake pamoja na mke wake Grace Mugabe.
Chanzo hicho kiliongeza kua hotuba yake ya jana ilipangwa na jeshi ili Mugabe atangaze kua kitendo hicho cha jeshi hakivunji katiba ya nchi hio ili kuondoa hali ya wasiwasi miongoni mwa wazimbabwe. Taarif
Tunachokifahamu mpaka sasa tangu hotuba ya jana.
>Mugabe bado ni raisi wa Zimbabwe baada ya kugoma kujiuzulu kwenye hotuba ya moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.
>Barua ya kujiuzulu ambayo inasemekana imeshaandikwa ni lazima imfikie kwanza spika wa bunge la nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment