KUUNDWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA "KUTOWEKA" KWA PALESTINA.
![]() |
Ramani ya mgawanyo wa maeneo kati ya Israel na Palestina [1948] |
![]() |
Jinsi ambavyo Israel na Palestina zilivyo kwa sasa |
Katika makala hii tutatazama kushamiri kwa mzozo kati ya Waisraeli na Palestina kuanzia 1948 hadi sasa. Hebu tuanze na haya maneno na badae itakusaidia kuelewa vyema.
Nakba ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha "Janga Kuu" yaani "Catastrophe". Lilitumika kuelezea vita ya 1948 kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake. Kuanzia 1998 siku hii imekua ikisherekewa kama kumbukizi kwa Wapalestina.
Ilikua tarehe 15.05.1948 ndio ukomo wa muda kwa Uingereza kua mwangalizi wa Palestina. Masaa manane kabla ya Uingereza kukomesha mamlaka yake katika nchi ya Palestina, Israel ilitangaza uhuru wake (14 May 1948). walitangaza muda huo kwa sababu ya kuiwahi Sabato kwa hio wasingetangaza siku ya Jumamosi (15.05.1948). Kumbuka Waisraeli wachache walikua wakiishi ndani ya Palestina.
Baada ya tangazo la Uhuru muungano wa nchi, za Kiarabu (Arab League) chini ya Misri ziliongoza vita dhidi ya taifa changa la Israel kuanzia 15 May 1948 hadi 10 Machi 1949 ambapo Israel walishinda.
Waarabu walichukia sana lakini walikua wakijipanga. Israel ilikuja kujichanganya 1956. Misri chini ya Abdel Gamal Nasser ilikua ndio tishio kubwa kwa taifa changa Israel na kumbuka wana Kisasi cha asili tangu miaka 400 ya utumwa.
Israel na tamaa ya kumdhibiti Egypt alilaghaiwa na Uingereza na Ufaransa kuipiga Egypt kila taifa likiwa na lengo tofauti; Israel alitaka usalama, Uingereza aliutaka udhibiti wa mfereji muhimu wa Suez (Nasser aliwafurusha Waingereza hapo) na Ufaransa ilitaka Misri isiidie Algeria katika vuguvugu la kumuondoa mkoloni (Mfaransa).
Katika sababu za kutatanisha uhusiano wa Israeli na Palestina tayari unajua kwamba ni asili na ahadi zao kimaandiko (Yakobo vs Ishmael), Eneo katika msingi wa Kijiographia na Kihistoria na Utambulisho (identity) kwa maana race na kwa kiasi flani dini! Ila kuna sababu unaona inaongezeka kuanzia 1956... Ubepari wa mataifa ya ng'ambo.
Hata hivyo Marekani ilizionya Uingereza, Israel na Ufaransa kutovamia Egypt na kutaka majeshi yao kuondoka mara moja. Kwa aibu kubwa mno Uingereza, Ufaransa na Israel zikaanza kutoa vikosi vyao kutoka Egypt na Gamal Abdel Nasser akawa mshindi na mwiba mkali wa Umajumui wa Kiarabu (Pan Arabism).
Naam tofauti na mtazamo wa wengi, dini imechukua sehemu ndogo hapa ila ujue dini ni zao la binadamu ndio maana kila mtu ana dini.
:::::::::::::::::::**
Vita baridi vilifanya Mashariki ya Kati kua kitovu cha siasa chafu. Misri na Syria wakiwa ni Washirika wakubwa wa Urusi na Israel akiwa mshirika mkuu wa Marekani.
Tatizo lilikuja 1967 ambapo Wàarabu waliazimia kuisambaratisha Israel lakini vita iliisha ndani ya siku sita tu. Nchi zote zilizoshiriki zilipigwa vibaya mno. Inabakia kua ndio kufeli vibaya zaidi kwa Waarabu dhidi ya Israel mpka leo. Israel alitwaa maeneo yaliyokua chini ya Jordan, Egypt na Palestina ikiwemo mji wa Yerusalemu.
Katika miaka ya 1970 Egypt akiwa kinara wa Waarabu aliongoza uvamizi dhidi ya Israel mwaka 1973 (Yom Kippur). Vita iliisha naweza kusema kwa ku sare. Sio Israel wala Egypt aliyeshinda ila kila mmoja aliathirika vibaya. Hii vita ilibadili sana mawazo ya Misri chini ya Anwar Sadar na kuamua kufuata njia ambayo ilikuja kufanya Misri kuchukiwa sana na Wapalestina na Waarabu wengine na ikaleta chachu ya kuzaliwa kwa HAMAS.
EGYPT ANATENGENEZA BOMU NA KUJILIPUA
Baba wa kutetea Waarabu hasa wa Palestina, shujaa na kiongozi mpendwa aliaga dunia 1970. Nae ni Gamal Abdel Nasser. Na sasa kiongozi mwingine shupavu ila mwenye maono ya mbali Amwar El Sadat anachukua madaraka. Akitaka amani kuliko vita ila alijua ni ngumu mwarabu na myahudi kuelewana. Lakini alijaribu akaweza. Aliipiganisha Israel vita ambavyo hakukua na mshindi wa wazi. Ilikua miaka 50 iliyopita kipindi kama cha sasa (1973).
Tukio lile lillilazimisha Israel na Egypt kumaliza tofauti zao. Majadiliano ya siku 12 chini ya Jimmy Carter rais wa Marekani kwa wakati huo ikapelekea kusaini majubaliano ya amani kati ya Egypt na Israel mwaka 1979 baada ya majadiliano ya huko Camp David, USA mwaka 1978.
Hii iliwachukiza saana Waarabu na wakati mmoja wakati Anwar Sadaat akiadhibisha siku ya Jeshi la Misri kuvuka Mfereji wa Suez (1973) na kuingia Sinai kwa mara ya kwanza tangu 1967, ndipo mwanachama mmoja wa kundi lenye mafungano na PLO aliamuua kumuua Anwar El Sadat mwaka 1981.
::::::::::::::****
Kupitia makubaliano hayo Misri ni wazi ilikikuka kila kitu kilichokubaliwa pale Khartoum mwaka 1967. (Imeelezewa sehemu ya tatu). Na sasa bomu lake hilo alilojitegea linamlupua na akafukuzwa uanachama Kutoka Arab League kwa sababu aliwasaliti Waarabu wote akalaaniwa vikali. Wapalestina wakakosa mtetezi wao wa Karibu.
HAMAS INAZALIWA
Sasa ikiwa Misri kafanya amani na Israel ni nani mwingine mwenye nguvu kupambana na Israel ? Hakuna. Imam mmoja anabadili historia ya kikundi kidogo cha misaada (Charity Group) kua kundi kubwa la mapambano dhidi ya Israeli. Naam! Hamas inazaliwa, vita zinaanza upya. Huku Hamas na pale Israel. Je, Kwanini HAMAS hapatani na Israel kabisa? Je Hamas ni wawakilishi wa Palestina kweli? Kwanini hawakubalini na sera za ndugu zao wa Palestinian Liberation Organization (PLO)?
![]() |
Wanamgambo wa HAMAS |
Itaendelea sehemu ya tatu.
Tutafurahi kupata maoni yako katika sehemu ya comment au enail au kwa SMS
Email: karlrck@gmail.com
SMS: 0787505800 WHATSAPP 0629293768
No comments:
Post a Comment