Tuesday, 24 October 2023

ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI?


Picha kwa hisani ya mtandao


ISRAEL NA PALESTINA NI MGOGORO WA KINABII AU ASILI? 

"Vita havina macho". Ni msemo tu katika jamii nyingi ukiwa na onyo la kutokushadadia vita. 

Tarehe 7 Oktoba 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi kwa saa za Israel, kulitokea shambulio la kushtukiza kutoka kikundi cha HAMAS ambacho kwa tafsiri ya Marekani na washirika wake ni kikundi cha kigaidi. 

Tukio hilo lilidhihirisha udhaifu katika idara ya ujasusi ya Israel kwa maana ya Mosad pamoja na Shin Bet. Kikubwa zaidi ni kile kilichokuja kuwa ni kisasi cha Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza.

Itoshe kusema mitaa mingi ya Gaza City imekua kama mji wa Kale uliokumbwa na kisa cha kutisha mno. Imekua kama "Ghost City". 

Tangu hapo kumekuwa na maoni tofauti juu ya nani yuko sahihi katika hili. Ukweli ni kwamba katika wakati huu ni swali baya ila kikubwa ni nani atasalia? Achilia mbali kua sahihi. 

HISTORIA FUPI YA MGOGORO

Eneo ambalo kwa sasa ni taifa la Israel ilikua zamani ikifahamika kwa majina tofauti lakini walau tunajua kua eneo hili lilifahamika kama Kanani. Nchi ya Ahadi ambayo Mungu aliitoa kwa Ibrahim na vizazi vyake [ Mwanzo 15:18-21]. Tunakumbuka kua hapo alipoahidiwa ndipo Ishmail(Yishmail) alizaliwa [Huyu ni baba wa asili ya Waarabu] na baadae Isaka na wengine. Hata Yakobo alipokea baraka zake kutoka kwa baba yake na Jina la Yakobo akapewa Jina ISRAEL likimaanisha kushindana na Mungu na wanadamu na kushinda. Mwanzo 32:25

Israel inapaswa kueleweka kua ni uzao ya Yakobo. Kulikua na watu wengine ambao sio wa Uzao wa Yakobo lakini waliishi hapo lakini jua walikua ni ndugu wa kabila nyingine kwa sababu ya uhusiano wao wazazi wa asili Mfano Ishmail na uzao wake na pia uzao wa Essau. 

Licha ya uteule wake, Israel ilifanya makosa na kupelekwa Utumwani nchini Misri. Baada ya miaka takribani 400 Mungu alikumbuka ahadi yake kwao. Aliwaokoa kupitia Musa. Ila kumbuka ni watu wawili tu waliotoka Misri na Kuingia Kanaani. Wengine wote walikua ni kizazi cha Pili. 

Walipofika walipigana vita kubwa mno na kuwashinda watu wa Babeli (Babylon) na kuvunja ukuta wa Jeriko. 

Walikaa hapo hadi walipovamiwa na utawala wa Dola La Kirumi (Roman Empire) katika miaka ya 63AD. Chini ya mateso ya Warumi walitawanyika kwenda maeneo mbalimbali. 

...........

WAPALESTINA NI NANI HASA? 

Ni vigumu kueleza asili ya moja kwa moja ya Wapelestina lakini Baba wa Historia duniani Mgiriki Herodotus katika maandishi yake ya karne ya 5 kabla ya kristo (KK) anataja eneo la kutoka Misri hadi Lebanon kama eneo la Palestina. Kwa lugha ya Misri ya Kale neno Palestina limetokana na neno "Peleset/Purasati" likimaanisha "Watu wakaao karibu na bahari (Sea Peoples)" hasa kwa wakati huo walikua ni Wafilisiti. Kwa sababu walipatikana mashariki mwa bahari ya Mediterania. 

Zingatia kua hawa Wapalestina wa mwanzo hawakua Waarabu na hawakua Waislamu! Naam, ndio hivyo. Lakini Wapalestina wa leo wengi ni Waarabu na ni Waislam. Na tuliona kua Wapelestina pamoja na Waarabu wengine ilikua ni uzao ambao nao ulibarikiwa kuanzia kwa Ishmail ambae aliahidiwa haya na Mungu. Ishmail[ Bwana Amesikia] atakua kama punda mwitu kati ya watu, mkono wake wake utakua juu ya watu wote na mikono ya watu wote juu yake. 

Ishmail alioa mke kutoka Misri na alikua hodari katika kuwinda na walikuja kukaa katika eneo la Parah katika Jangwa la Shuri [Eneo la Misiri, Kanaani na Sinai].  

Na inasemekana Wafilisti walifika eneo la Kanaan zamani sana labda miaka 1175 KK. Walikua watu wenye nguvu na fujo. Walifanya vita na watu wa Kanaan ikiwemo Wayahudi. 

Lakini baada ya kukaa kwa muda mrefu utawala wao uliharibiwa na Mfalme Nebukadneza II na kupoteza utambulisho wao. Hata hivyo, huenda baada ya hapo ndipo watu waliokuja waliingiliana na badae Wapelestina Waarabu wakatokea kwa sababu walikaa eneo lile la Pwani ya Bahari ya Mediterania na tangu mwanzo hawakuelewana na ndugu zao ambao ni Wayahudi. 


Picha kwa hisani ya mtandao

ISRAEL NA PALESTINA ZA KALE NA SASA. 

Tumeona pasina shaka kua tangu mwanzo Wayahudi sio tu wa dini bali wa utamaduni na asili na Wapalestina si tu kwa sababu ya dini yao ila kwa sababu ya eneo lap walilopatikana. Na walifanya vita kubwa na hadi tunaona katika Biblia kua Daudi alimua Goliati ambae alikua ni Mfilisti. 

Lakini tunaona Wapelestina hawajahamia hapo walipo.. walikuepo na Wayahudi walikuepo lakini walipewa eneo pia kwa ahadi ya Mungu ambapo wengine sasa ikiwemo wapalestina wanakosa hio ahadi. Hapo tu ndio kunatofauti. Tukitoa ahadi, kila mtu anauhalali wa kihistoria na eneo hilo. 

Baada ya mtawanyiko wa waisraeli nchi ya Palestina iliendelea kuwepo na wapalestina pia. 

KARNE YA 20

UCHOCHEZI WA UINGEREZA KATIKA MGOGORO NA CHANZO CHA VITA VISIVYOISHA 

Wanasema "Hakuna dola isiyoanguka". 

Mwaka 1299A.D Dola kubwa chini ya Uislam liliweza kuanzishwa na kulishinda dola la Kirumi. Hili sio jingine bali ni OTTOMAN EMPIRE. Hapa eneo la Israel na Palestina lilikaliwa na Wapelestina ambao ni Waislam. 

Mnamo 1850s Ottoman ilikua dhaifu sana na mataifa makubwa ya Ulaya waligombania baadhi ya Maeneo. Uingereza ilijipatia Ushawishi mkubwa saana. Wakati wa vita vya kwanza vya dunia (1914-1918) Uingereza iliweza kua na Ushawishi mkubwa katika Ottoman Empire. Kumbuka Wayahudi wengi waliishi humo. Ottoman Empire iliunga mkono Ujerumani hasimu mkuu wa Uingereza katika vita. 

Ili kushinda vita, Uingereza ilitoa ahadi mbili zinazofanana kwa watu wawili wasiofanana na imekua ni mwiba wa kile kinachoendelea leo kati ya Israel na Palestina. Hili ni moja ya kosa kubwa la Uingereza katika Mashariki Ya Kati. 

Nadhani ni wazi kusema Uingerez kwa kujua na kutarajia au kujua bila kutarajia alitengeneza mgogoro huu. Na hapa naungana Theo Hotz ambae ni mwanahistoria mashuhuri pia ameona namna Waingereza waliweza kua wa kutiliwa mashaka kwa ahadi zao. 

Mawasiliano ya McMahon-Hussein (Huyu Alikua ni Kiongozi mwenye Ushawishi katika eneo la Urabuni) na Azimio la Balfour, zote kutoka Vita vya Kwanza vya Dunia.

Sehemu ya maelezo ya Hotz na BBC

Kwa upande mmoja, kulikuwa na ahadi ya Uingereza "kuunga mkono na kutambua uhuru wa Waarabu huko Palestina". Kwa upande mwingine, "kuundwa kwa makazi ya kitaifa kwa watu wa Kiyahudi katika eneo la kijiografia la Palestina".


"Waingereza waliahidi jambo lile lile kwa watu wote wawili," asema Hotz.

Kwa hio Waarabu na Wayahudi waliahidiwa kitu kile kile. Baada ya vita kuisha kulikua na uhasama kiasi kati ya Waarabu dhidi ya Uingereza lakini kuanzia 1920 Palestina ilikua chini ya Uingereza. Katika miaka ya 1930s Uingereza iliunda tume mbili za kuchunguza na kushauri mustakabali wa Waarabu wa Palestina na Wayahudi. Tume zote mbili zilipendekeza kuundwa kwa taifa la Israel ndani ya Palestina. 

Mnamo 29 Novemba 1947 Umoja wa Mataifa (UN) ulipitisha azimio UN Resolution 181 (II) Mpango wa Kuigawanya Palestina. Mataifa 33 yaliunga mkono, mataifa 13 yote ya Kiarabu yalipinga na mataifa 10 ikiwemo UINGEREZA YALIJIZUIA KUOIGA KURA! 

Tarehe 14 May 1948 ndipo utawala wa Uingereza ulikua unakoma Palestina. Na tarehe 14 May 1948 majira ya 12 jioni chini ya David Ben-Gurion ndio siku ambapo Israel ilijitazia kuundwa kwa taifa lake katika Ardhi ya Palestina.  

Uingereza ameondoka akiwa amevunja ahadi yake kwa Waarabu ya mwaka 1915 na ahadi yake kwa Israel ya mwaka 1917. Na kwa sababu ameondoka akiwa hajabariki kuundwa kwa Israel kama alivyoahidi 1917 kwa sababu hakupiga kura ya kuunga mkono azimio la 1947 ni wazi alitoa mwanya kwa Wapelestina kuanzisha vita vya kupinga 

Kuanzishwa kwa Israel. 

Baada ya azimio kupita na kuundwa kwa taifa la Israel ni kinakwamisha mchakato wa kua na mataifa mawili hapo? Ni dini? Asili ya watu au kuna jambo jingine kubwa? 

Unajua nini kilitokea kuanzia siku ya tarehe 14 May 1948? Nani aliungana na nani? Je ni dini au eneo? Tukutanane tena wakati mwingine.

Itaendelea......... 



1 comment:

  1. Well detailed article. Keep it up blogger 👍

    ReplyDelete