Posts

KIJANA MMOJA AUWA KWA KUPIGWA NA MWEKEZAJI.

Image
Kijana mmoja aliyejukikana kwa jina moja (Elisha) mkazi wa Kabindi Mkoani Geita amefariki Dunia baada ya kupigwa na mchina kwa jina "Mr. Swii" kwa madai ya kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara. Taarifa zinadai waliopigwa wengine wawili wako hospitali kwa matibabu zaidi.

WALINZI ZAIDI YA 300 WA KIKOSI CHA KUMLINDA RAISI KUKAMATWA UTURUKI.

Uturuki imetoa warrant wa kukamatwa kwa zaidi ya walinzi 300 wa kikosi cha kumlinda raisi kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli tarehe 15 July 2016. Inasemekana tayari walinzi 283 tayari wameshakamatwa na operesheni hio ingali bado inaendelea, liliripoti shirika la habari la Xinhua.

MLEMAVU APANDIKIZWA MIKONO YA MTU MWINGINE.

Uingereza imefanikiwa kufanya upasuaji na kumpandikiza mgonjwa mikono ya mtu mwingine. Oparesheni hiyo imefanyika katika hospitali kuu ya Leeds ambako mgonjwa mwenyewe amesema amefurahia kurudishiwa viungo hivyo muhimu mwilini.

ULIIKOSA HII YA KOFFI OLAMIDE AKIMPIGA TEKE DENSA WAKE?

Image
Msanii Koffi Olamide amenaswa na kamera akimpiga teke densa wake wakati wanawasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini kenya.

MAGARI YA UMEME YAANZA KUUZWA KENYA.

Image
Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.

VYUO VILIVYOFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Image
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/17.

JE, TUNAWEZA KUEPUKA MALARIA KWA KUFUGA KUKU? SOMA UTAFITI HU.

Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ? Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,, Fuga kuku ! Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.