Saturday, 23 July 2016

WALINZI ZAIDI YA 300 WA KIKOSI CHA KUMLINDA RAISI KUKAMATWA UTURUKI.

Uturuki imetoa warrant wa kukamatwa kwa zaidi ya walinzi 300 wa kikosi cha kumlinda raisi kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli tarehe 15 July 2016.
Inasemekana tayari walinzi 283 tayari wameshakamatwa na operesheni hio ingali bado inaendelea, liliripoti shirika la habari la Xinhua.


Wakati huo huo zaidi ya hati za kusafiria 10,000 zimezuiliwa kutokana na hatari ya kutoroka nchi. Shirika linaloongozwa na serikali la Anadolu liliripoti kua jana ijumaa kua zaidi ya wafanyakazi 44,000 wa taasisi za serikali wameachishwa kazi au kushtakiwa kwa kuhusishwa na madai kua walishiriki katika jaribio la mapinduzi lililopangwa na kiongozi wa dini aishiye marekani, Fethullah Gulen. Waziri wa elimu alitangaza kuwasimamisha kazi watumishi 21,738 huku kati yao 21,029 wakiwa ni walimu. Majaji wa mahakama za kijeshi na waendesha mashtaka zaidi ya 262 pia wameachishwa kazi.

No comments:

Post a Comment