Kwa miaka mingi sasa kumekua na mijadala mikubwa kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya simu. Matumizi ya simu yamekua yakiongezeka kila kukicha. Sasa watu wanatuma ujumbe wa maneno, sauti,video, kuchati kwenye mitandao ya kijamii, kutazama video mtandaoni, kutumiana picha, kuperuzi, kusoma vitabu, majarida n.k kupiga picha za selfie n.k yote haya ni matumizi ya simu lakini swali kubwa linabaki "Je ni kweli matumizi ya simu hayana athari zozote kiafya?".
Madhara ya simu ni pamoja na haya baadhi ni madogo ila mengine ni makubwa.
1. Uchafu.
Kutokana na takwimu za kisayansi simu iliyotumika mara nyingi zaidi ina uchafu mara 10 zaidi ukilinganisha na sink la chooni!! Huamini sio?? Fikiria ni mara ngapi umejisumbua kusafisha simu yako baada ya kutoka chooni, kumshika mbwa,paka, kufanya usafi wa chumba au nyumba yako? Baada ya kushika mavumbi?? Sasa basi uchafu huo wote ulioko mikononi huhamia kwenye kioo cha simu yako. Wanasayansi wamegundua kua simu ina uwezo wa kuhifadhi bakteria aina ya E.coli ambao wana uwezo wa kusababisha homa, kutapika, na kuhara. Kuepuka hili na kuzuia bakteria kusambaa unashauriwa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni pia kusafisha simu yako kwa kutumia "Antibacterial wipe".
2. Hatari ya kifo wakati wa kutafuta maeneo mzuri ya kupigia picha.
Hii sio mara moja au mbili, watu wengi wameshakufa wakijaribu kupiga picha kwenye maeneo hatarishi. Kuna watu wanapiga picha barabarani wanagongwa, wengine kwenye maeneo yaliyozuiwa kama karibu na maporomoko, magema n.k. Idadi ya vifo vitokanavyo na matumizi ya simu inatisha sana kwa sasa.
3. Kuchati na au kuongea na simu wakati unaendesha.
Inaweza kuonekana kama jambo la ajabu lakini simu husababisha ajali karibu milioni moja na laki sita kila mwaka ambapo zaidi ya watu nusu milioni huumia na wengine zaidi ya 6000 hupoteza maisha.
4. Uoni hafifu.
Madaktari na hasa wataalamu wa macho wamekua wakionya kua matumizi makubwa ya simu, tablets, kompyuta na TV yanasababisha matatizo ya macho. Karibu theluthi moja ya watu wazima wanaotumia vifaa vya kielektroniki kwa masaa sita au zaidi kwa siku wanasumbuliwa na uoni hafifu, macho kua mekundu, kuwasha, maumivu nyuma ya kichwa, maumivu ya shingo na kichwa.
Kwa weka kifaa chako mbali kidogo kutoka kwenye macho yako.
5. Uwezekano wa kupata kansa.
Bado wanasanyansi hawajaweza kuthibitisha kuwepo kwa kansa itokanayo na matumizi ya simu lakini kuna kila sababu kua huenda vifaa vya mawasiliano vikahusika kusababisha kansa na hasa kansa ya ubongo na pia mawimbi ya sauti ya vifaa hivi huenda yana madhara na hili swala linahitaji utafiti wa kina na pia ni vema watoto wakaepushwa katika matumizi ya simu.
Tutumie simu kwa tahadhari. Share ujumbe huu kwa wenzako.
No comments:
Post a Comment