Saturday, 13 August 2016

MESI AKUBALI KURUDI TIMU YA TAIFA.


Nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Mesi ameamua kubadili uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu yake ya Argentina kufuatia matokeo mabovu ya timu yake kwenye fainali za michuano mikubwa. Mesi alifikia uamuzi huo kufuatia mazungumzo kati yake na kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza.


Mesi alithibitisha uamuzi wake huo wa kurudi katika soka la kimataifa ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu kumalizika kwa fainali za Copa America za mwaka 2016. Baada ya mazungumzo na bosi wake mpya, Edgardo Bauza alisema Mesi amefikia uamuzi wa kurudi kuitumikia timu yake ya taifa kwa mara nyingine tena.

"Naona kuna matatizo mengi kwenye timu ya Argentina na mimi sitaki kuongeza hata moja", alisema kwenye taarifa iliyotolewa jana Ijumaa. "Tunapaswa kurekebisha vitu vingi kwenye mpira wa Argentina, lakini ni bora kufanya hivyo nikiwa ndani kuliko kua kukosoa kutoka nje". Nahodha huyo alieleza kua ni mapenzi yake kwa timu yake ya taifa ndio yaliyomsababisha kurudi kuichezea timu hiyo kwa mara nyingine tena.

No comments:

Post a Comment