Sunday, 3 November 2019

MAAJABU YA JAPANI




Image result for attraction icon for japan
Photo credit: the crazy tourist.com

Kuna mambo mengi hutokea duniani na katika jamii flani yakiwa na upekee kabisa kutoka upande au pande nyingne za dunia. Na Japan ni moja ya mataifa ambayo kwa kiasi kikubwa kuna vitu flani ambavyo hatujavizoea katika sehemu nyingne nyingi.

Ikiwa ni moja kati ya nchi tajiri kabisa duniani ikiwa nyuma ya China na Marekani hebu tazama vitu ambavyo Japan wana vifanya tofauti na seehemu nyingine.

Tuesday, 29 October 2019

KUMBUKIZI YA KIFO CHA GADDAFI

Ilikua huko katika mji wa Sirte alizaliwa mwana wa kiume kama Muammar Mohammed Abu Minyar al-Gaddafi na baadae alifahamika kama Colonel Muammar Gaddafi kiongozi wa Libya kati ya September 1, 1969-October 20, 2011. Alikua ni Mlibya mmoja mwenye asili ya kitaliano aliyezaliwa na kukuzwa katika mazingira ya kimaskini katika nchi maskini ya Libya.

Wednesday, 19 June 2019

KIM JONG UN NA XI JINPING KULIKONI?

BEIJING, CHINA.
Katibu mkuu wa chama cha kicomusti nchini china (communist party of china-CPC) na rais wa nchi hio Xi jin Ping wanatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Korea ya Kaskazini kati ya Juni 20-21 mwaka huu ikiwa ni mwaliko wa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un. taarifa hii ni kwa mujibu wa idara y habari ya chama cha CPC iliyotolewa jana jumatatu. 

Tuesday, 18 June 2019

JE, MATAIFA YA ULAYA YANA MPANGO WA KUITOSA MAREKANI?

Suala la ulinzi na usalama ni moja ya mambo makubwa na muhimu ambayo kwa kipindi kirefu yamekua yakisumbua vichwa vya watunga sera na viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali makubwa duniani. kufuatia vitisho vya vya uliokua muungano wa Soviet ulipelekea kuundwa kwa Umoja wa kujihami wa NATO mwaka 1949 na baadae muungano wa Soviet uliunda umoja wake wa Warsaw Pact mwaka 1955.