KUMBUKIZI YA KIFO CHA GADDAFI.
Muammar Gaddafi alibahatika kwenda shule huko Sabha na baadae alienda kujiunga na Royal Military Academy huko Bengazi. Akiwa huko basi alianzisha kikundi chake chake kimapinduzi kilichokuja kufanya mapinduzi ya Libya. Huko pia alikuza falsafa zake zilizoshabihiana na zile za vuguvugu la kujenga utaifa ndani ya nchi za kiarabu (Arab Nationalism).
Muammar Gaddafi alialikua ni kiongozi wa Libya na alipata uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka 1969 akiwa kijana mdogo wa miaka 27 pekee aliyekua kanali wa jeshi la Libya. Aliupindua utawala uliopigiwa chepuo na mataifa ya kibeberu kama Marekani, Ufaransa na Uingereza uliokua chini ya Mfalme Idris I.
Akiwa mdogo Gaddafi alikua mtu makini japo mda mwingi aliutumia akiwa mwenyewe akifanya mambo yake ya msingi. Baada ya kumpindua mfalme Idris I, Gaddafi aliibadili Ufalme wa Libya kua Jamhuri ya Libya Jamahiriya (1977) na alikua muumini wa falsafa ya tatu ya kimataifa(The International Theory) ambayo ilipingana na sera za kibepari na zile za Ukomunisti. Maendeleo mengi yalifikiwa chini ya uongozi wa Muammar Gaddafi.
Ijapo hakua na mahusiano mazuri mataifa ya magharibi hasa juu ya mpango wake wa nuklia ila alifanikiwa kuiendeleza Libya licha ya vikwazo vya mabepari. Baada ya George Bush kuivamia Iraq basi Gaddafi alihofia dhahma kama ile kua ingemkumba na hivyo akaamua kuanzisha uhusiano mzuri na mataifa ya magharibi kwa masharti kua ataondolewa vikwazo. Hayo yalifanyika mwaka 2004. Kuanzia hapo Libya ilistawi zaidi kutoka nchi maskini na kua nchi ya kwanza kwa uchumi wa kichwa cha mtu mmoja mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali mpka Gadafi anauwawa Libya ilikua haidaiwi, kulikua na huduma bure za kijamii, malipo kwa wasio na kazi na kiasi cha fedha za mafuta wananchi walinufaika nazo moja kwa moja.
Licha ya mafanikio haya, kuanzia mwaka 2010 kulikua na vuguvugu la mapinduzi ya waarabu maarufu kama (Arab spring revolution). Mapinduzi hayaligusa pia Libya vikosi kadhaa viliibuka na kuupinga utawala wa Kanali Muammar Gaddafi. Baadae vikundi vya uasi vikafadhiliwa na nchi za magharibi chini wa mwamvuli wa Umoja kujihami wa nchi za magharibi wa NATO ili kumuondoa Gaddafi madarakani. Aliapa kuilinda na kuitetea Libya mpka mwisho na aliapa kwamba hatokimbia ila atafia Libya.
Baada ya mapigano makali katika mji wa Benghazi na Tripoli, Muammar Gaddafi alitaka kukimbilia katika mji wa Sitre alikozaliwa. Safari ile inakua ni sehemu muhimu katika utawala wa Kanali Muammar Gaddafi na historia ya Libya kwa ujumla. Akiwa njiani kuekea Sitre msafara wake ulishambuliwa na waasi wakisaidiwa na ndege zisizokua na rubani (Drones). Alipojua kua hawezi kukimbia aliingia na kujificha mtaroni ambapo waasi walifanikiwa kushika.
Aliteswa sana, alilia sana na kati ya maneno aliyoyaongea yalikua ni "kwani nimewakosea nini"?. Aliuliza hivyo kwa kua alifanya yote kwa walibya kasoro UHURU tu ndio walikua hawana. Baada ya mateso kadhaa inasemekana alipigwa risasi ya tumbo kwa mujibu wa ripoti ya daktari. Lakini ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2012 inasemekana alijeruhiwa na bomu la kurusha kwa mkono kutoka miongoni wa walinzi wake ambaye alijaribu kurusha bomu lakin likagonga kwenye ukuta na kurudi.
Inasemekana pia mazishi yake na mwanae yalifanyika tarehe 25 October 2011 katika eneo lisilofahamika huko jangwani. Huo ukawa mwisho wa COLONEL MUAMMAR GADDAFI mwana wa Afrika. Afrika tuna mengi ya kujifunza kupitia Muamar Gaddafi.
No comments:
Post a Comment