Wednesday, 19 June 2019

KIM JONG UN NA XI JINPING KULIKONI?

BEIJING, CHINA.
Katibu mkuu wa chama cha kicomusti nchini china (communist party of china-CPC) na rais wa nchi hio Xi jin Ping wanatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Korea ya Kaskazini kati ya Juni 20-21 mwaka huu ikiwa ni mwaliko wa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un. taarifa hii ni kwa mujibu wa idara y habari ya chama cha CPC iliyotolewa jana jumatatu. 

Hii itakua ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu ya CPC na rais wa China kuitembelea korea kaskazini katika kipindi cha miaka 14. mualiko huu unakuja ikiwa China na Korea Kaskazini zinaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo jirani ya bara la Asia. Tangu zamani China na Korea zimekua zikishirikiana katika baadhi ya mambo licha ya kua kuna wakati wanatofautiana juu ya mambo lakini tofauti zao hua si kubwa.
Hii inakua ni mara ya nne kwa viongozi hao kukutana ikiwa mara tatu zilizopita Kim Jong Un ameitembelea China na mara ya mwisho ilikua in mkutano wake na Xi Jin Ping mwezi Januari mwaka huu. Na pia Xi Jin Ping anakua kiongozi wa pili mkubwa kutoka nje kukutana na Kim tangu kuvujika kwa mkutano wa Kim na Trump mwezi Februari mjini Hanoi nchini Vietnam.
katika mazungumzo hayo viongozi hao watajadili uhusiano wao katika miaka 70 iliyopita, maendeleo ndani ya nchi zao na namna nchi hizo zinavyoweza kuboresha uhusiano wao kwa anufaa ya mataifa yao.
Swali la msingi la kujiuliza ni kwanini rais Kim Jong Un amekua na mazungumzo ya mara kwa mara na viongozi wa mataifa makubwa duniani? Haya yanajiri huku kukiwa na ripoti kutoka mashirika mbalimbali kwamba mamilioni ya watu nchini Korea Kaskazini wanakabiliwa na baa lanjaa. Je, bwana Kim anajaribu kuinusuru Korea au anaiweka rehani?

Cc: Xinhua

Unaweza kutuandiki ujumbe wako katika kisanduku hapo chini. 

No comments:

Post a Comment