Sunday, 3 November 2019

MAAJABU YA JAPANI




Image result for attraction icon for japan
Photo credit: the crazy tourist.com

Kuna mambo mengi hutokea duniani na katika jamii flani yakiwa na upekee kabisa kutoka upande au pande nyingne za dunia. Na Japan ni moja ya mataifa ambayo kwa kiasi kikubwa kuna vitu flani ambavyo hatujavizoea katika sehemu nyingne nyingi.

Ikiwa ni moja kati ya nchi tajiri kabisa duniani ikiwa nyuma ya China na Marekani hebu tazama vitu ambavyo Japan wana vifanya tofauti na seehemu nyingine.




1. TRAFFIC LIGHTS
Wakati kwingineko duniani taa za kuongozea watumiaji wa barabara zina rangi nyekundu, njano na kijani. kwa Japan wao wana nyekundu, njano na bluu! yes wao wanatumia bluu badala ya kijani.

Image result for traffic lights in japanImage result for traffic lights in japan



2.  KULALA KAZINI/MUDA WA KAZI.
Wakati sehemu nyingi ukilala muda wa kazi inahesabika kama ni uvivu na wakati mwingine inaweza kukugharimu hata kazi yako, ila Japan hali ni tofaaaauti kabisa kwani ukilala kazini unaonekana wewe ni mchapa kazi haswa! na wakati flani mtu akilala huzawadiwa na hii inapelekea wafanyakazi wengi Japan kujifanyisha wamelala.
Image result for workers sleeping on job in japan

3. NI NADRA KUONA MTU ANAKULA CHAKULA PEKEE YAKE MGAHAWANI.
Na hata inapotekea hili basi wahudumu hutafuta mdoli mkubwa na kumuweka karibu na mteja ili asijihisi kama yuko mwenyewe. Japo pia kuna utamaduni wa kufanya watu wa focus kwene kula ikitokea hivi watu hutengwa na wenzao ili waweze kula na kumaliza chakula walichoandaliwa.


4. WAJAPANI WANAAMINI NO.4 INA MIKOSI
Ni nadra kuona vitu vikiwa vimekaa vinne katika maisha ya watu wengi pale Japan kwa kwao sio namba ya bahati. mfano kama mmekutana na marafiki sehemu ila mkajikuta mko wanne mmoja inabidi aondoke au aongezeke. Hii hata ukipand elevator (lifti) hauoni kitufe cha ghorofa ya nne. Sababu kubwa inasemekana namba 4 inaandikwa na kutamkwa sawa na kifo yaani "Shi"
Image result for why japanese avoid number 4 Image result for why japanese avoid number 4

5. UMBRELLA PARK
Japan katika majengo makubwa ya umma na hata ya binafsi kumewekwa maeneo maalum ambayo watu wanaweza kuweka miavuli yao na pia watu hawachukuliani miavuli hio.

Image result for umbrella park in japan
Cc:Bright

No comments:

Post a Comment