Posts

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI RUFAA YA TRUMP.

Image
Mahakama ya rufaa nchini Mareni imekataa ombi kutoka kwa idara ya haki nchini humo la kutaka kurejeshwa amri ya Trump ya kupiga marufuku wasafiri kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

SHULE IMEFUNGA CCTV CAMERA KUDHIBITI NIDHAMU YA WANAFUNZI.

Tafakari haya, ndani ya shule ya upili, kuna kamera zilizotundikwa katika kila pembe ya shule ili kuboresha nidhamu. Mwanafunzi anapokiuka sheria na kanuni za shule basi hana lake kwani ushahidi utanaswa kwenye kamera. Ndivyo mambo yalivyo katika shule ya upili ya wavulana ya Karima katika eneo la Othaya. Isitoshe, kando na kamera hizo, kuna mashine zinazotambua alama za vidole za mwanafunzi na kutuma ujumbe mfupi kwa mzazi iwapo mwanafunzi huyo anaingia au kutoka shuleni. Lakini jambo kubwa la kujiuliza ni je hii ni njia sahihi ya kudhibiti nidhamu ili kama inafaa basi shule nyingine pia ziige mfano huu kwenye maeneo yetu?  Unaweza kuandika maoni yako kwenye blog au kwenye tweeter na facebook. 

MAREKANI YAIONYA IRAN KWA KUIWEKEA VIKWAZO VIPYA.

Image
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora. Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016

Baraza la mitihani la taifa limetoa matokeo ya kidato cha nne 2016. Kuangalia matokeo bonyeza hapa>>> http://tanzania.go.tz/result_csee_2016/CSEE_2016/index.htm

MBARONI KWA KUANZISHA BENKI BANDIA.

Image
Mahakama mjini Nanjing, China, imewafunga jela wanaume wawili waliowatapeli wateja kupitia benki bandia, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Wanaume hao waliotambuliwa kwa majina Zeng na He, walipatikana na makosa ya kujipatia yuan 435m (£51m; $63m) kutoka kwa wateja 400.

KUTANA NA MARAIS "VIPANGA"KUTOKA AFRIKA.

Image
KUTANA NA MARAIS WALIO BUKUA KWA SANA(VIPANGA) KUTOKA AFRIKA. Sio tu kua hawa viongozi wana nguvu na ushawishi kisiasa bali ukiangalia taaluma zao pia ziko juu sana. Wana weledi mkubwa kitaaluma na hawa wanatuthibitishia ule msemo wa kiingereza usemao "readers are leaders". Orodha hii imepangwa kulingana na vigezo vyao vya kitaaluma.

NCHI ZINAZOONGOZA KUA NA "VIPANGA" SHULENI.

Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?