MWALIMU MKUU/ HEADMASTER SEHEMU YA TATU Baadae nilimskia mwalimu mkuu kua anataka kupumzika...kila mwamafunzi alifurahi kwa kua aliamini atasoma kwenye shule aliyokua akiiota.. Endelea...
Picha ya pamoja ya viongozi wa Ulaya na Rais wa Marekani ikulu ya Marekani tarehe 18 Agosti 2025. Picha na AFP February 2022 Urusi iliivamia Ukraine kijeshi katika kile ambacho Moscow walikiita kama Operesheni Maalumu (Special Operation). Na tangu wakati huo vita hio imeendelea na dalili za kukoma kwake bado zinaonekana ziko mbali kulingana na matokeo ya jitihada mbalimbali za kukomesha vita hivyo. Lakini kwa sasa vita vimeingia katika hatua muhimu na huenda ni hatua mbaya sana ambayo kosa kidogo la kimahesabu limaweza kuigharimu dunia kama ilivyokua Julai 1918 au Septemba 1939 ambapo vita vya kwanza na pili vilianza mtawalia. Kwa sasa vita vya Ukraine vina sura ya tofauti ambayo inahatarisha usalama wa dunia. Na haya ndio mambo ya hatari zaidi ambayo yanaweza kushindwa kuzuilika na kuleta vita ya tatu ya dunia.
Picha za smartphone mbalimbali Miongoni mwa masoko magumu kwa sasa ni pamoja na soko la simu janja au rununu (smartphones) ambapo kila kampuni ya utengenezaji wa siku inajitajidi kutoa simu zenye ubora wa hali ya juu. Lakini sio rahisi kama unavofikiria ikiwa utaulizwa ipi ni simu bora kwa sasa sokoni. Kwa sababu simu moja kutoka kampuni flani inaweza kua bora kwenye eneo moja au mawili hivi lakini ikashindwa kua bora katika maeneo mengine. Lakini kati ya vitu virahisi na hua ni kigezo cha watu kununua simu hua ni kamera. Hii hapa ni orodha ya simu 10 zenye kamera bora sana mpaka sasa.
AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? HATIMAYE AFRIKA IMEANZA KUZINDUKA. Ramani ya dunia Tulipokua shuleni tulijifunza mengi juu ya Afrika lakini mengi ilikua ni upotoshaji wa kukusudia au kutokukusudia. Hilo linajidhihirisha pale unapotazama ramani ya dunia. Utaambiwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani nyuma ya Asia lakini ukitazama ramani utagundua Amerika ya Kaskazini inaonekana kuwa ni kubwa kuliko Afrika. Lakini je Afrika ina ukubwa gani? Na kwanini sasa Umoja wa Afrika unahitaji taasisi kuu ulimwenguni kote kutumia ramani mpya ya Afrika kulikoni? Tunarejea takribani miaka 456 hivi nyuma kuanzia sasa. Tunakutana na mwaka 1569, na hapo tunakuja kukutana na mtu mmoja aliyepata kua ni mwanajiografia na mchora ramani kutoka Flanders (Kijiografia eneo hili liko Ubelgiji na kijamii na kiutamaduni limekaliwa na watu asili ya Wadachi). Mtu huyu alitwa Gerardus Mercator ambaye ndiye aliyechora ramani hii ya dunia ambayo katika karne ya 18 ilirasmishwa kutumika katika maswala ya usa...
Comments
Post a Comment