Friday, 3 February 2017
MAREKANI YAIONYA IRAN KWA KUIWEKEA VIKWAZO VIPYA.
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora.
Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.
Rais Donald Trump aliandika mapema kwenye mtandao wa twitter kuwa,"Iran inacheza na moto, hawana shukran jinsi Obama alikuwa mkarimu kwao, Si mimi!"
Lakini Iran inasema kuwa hauwezi kulegeza kamba kutokana na vitisho visivyo na maana vya Marekani, kutoka kwa mtu asiye na ujuzi.
Kati ya makudi yaliyowekewa vikwazo yako nchi ya miliki za kiarabu , Lebanon na China.
Wiki hii mshauri wa masuala ya ulinzi Michael Flynn, alisema kuwa Marekani inaionya Iran kufuatia jaribio hilo la kombora.
Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni kwa Iran Mohammad Javad Zarif, leo Ijumaa aliandika kwenye mtandao wa twitter akisema kuwa Jamhuri hiyo ya kiislamu haitikiswi na vitisho vya Marekani.
Alisema kuwa Iran haina mipango yoyote ya kutumia jeshi lake dhidi ya nchi yoyote bali kujilinda.
Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya marekani kwa vyombo vya habari inaeleza kua imewawekea vikwazo watu binafsi na makampuni ishirini na tano ambao wanaunga mkono hatua za kinyuklia za Iran. Taarifa hiyo inaeleza kua jumuiya ya kimataifa kupitia baraza lake la usalama la umoja wa mataifa wamekua wakiivumilia sana Iran ila kwa sasa muda wa uvumilivu umekwisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment