KUTANA NA MARAIS WALIO BUKUA KWA SANA(VIPANGA) KUTOKA AFRIKA.
Sio tu kua hawa viongozi wana nguvu na ushawishi kisiasa bali ukiangalia taaluma zao pia ziko juu sana. Wana weledi mkubwa kitaaluma na hawa wanatuthibitishia ule msemo wa kiingereza usemao "readers are leaders". Orodha hii imepangwa kulingana na vigezo vyao vya kitaaluma.
1. MFALME MOHAMMED VI(MOROCCO).
Huyu ni mfalme wa Morocco ambaye alimrithi baba yake mwaka 1999.
√Alimaliza shule ya msingi na sekondari katika shule ya Royal college. Alipata shahada ya kwanza ya sheria kwenye chuo kikuu cha Mohammed V huko Agdal.
√Alipata alisomea sayansi ya siasa kwa ngazi ya cheti (CES) na baadae alipata stashahada ya sheria ya umma.
√Alipata shahada ya uzamivu (PhD) kutoka chuo kikuu cha Ufaransa huko Nice( French university of Nice).
Na huyu ataizuru Tanzania hapo jumapili ya tarehe 25.
2. DR PETER MUTHARIKA(MALAWI)
Huyu ni rais wa malawi na mcheki kisomo chake hapa.
√Alipata shahada ya sheria(LL.B) kutoka University of London na alienda kupata shahada ya pili(master's) (LL.M) na Udaktari wa sayansi ya sheria kutoka chuo kikuu cha Yale.
3. ALASSANE QUATTARA(COTE D' IVOIRE)
Alikua ni rais wa Ivory coast kuanzia mwaka 2010.
√Alisomea shahada ya sayansi kutoka chuo kikuu cha Drexel institute of Technology, Pennsylvania.
Pia alipata shahada ya umahiri (master's) na shahada ya uzamivu( Phd) ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Pennsylvania.
4. Dr MULATU TESHOME(ETHIOPIA).
√ Huyu kasomea China. Alipata shahada ya kwanza katika falsafa ya siasa-uchumi na pia alisomea udaktari wa sheria za kimataifa kutoka chuo kikuu cha Peking.
5. Dr AMEENAH GURIB (MAURITIUS)
Mwanamke wa kwanza kua rais wa Mauritius. Alipata shahada ya sayansi katika kemia kutoka Surrey University, Uingereza.
√Alipata shahada ya uzamivu (PhD) ya organic chemistry kutoka Exeter University.
6. IBRAHIM BOUBACAR KEITA (MALI).
√ Ana master's ya sayansi ya siasa, master's ya historia kutoka LycĂ©e Askia-Sailly, Paris.
√Pia ana shahada ya sayansi ya siasa na sheria ya kimataifa kutoka Dakar university.
7. ROBERT MUGABE(ZIMBABWE).
Huyu jamaa unaweza kumuita mchawi wa kitaaluma.
Ana master's ya sheria(LL.B), ana master's ya sayansi(M.Sc), shahada ya sheria(LL.B), shahada ya sayansi(B.Sc), shahada ya elimu(ualimu)(B.Ed), shahada ya utawala(B.A.A), Shahada ya sanaa(B.A).
8. FAURE GNASSINGBE(TOGO)
√ Alipata shahada ya usimamizi wa biashara na fedha kutoka Paris, na master's ya usimamizi wa biashara(MBA) kutoka The George Washington university. Shahada ya biashara.
9. ELLEN JOHNSON SIRLEAF(LIBERIA)
Alikua ndio rais pekee wa kwanza mwanamke kuchaguliwa katika bara la afrika mwaka 2006.
Ana shahada ya utawala wa umma(B.P.Adm), master's ya utawala wa umma(M.P.Adm.), shahada ya uchumi(BEc), na shahada ya uhasibu (A.A).
Usisahau ku share na wenzako hii,
No comments:
Post a Comment