TAMKO MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUKEMEA UKIUKWAJI WA HAKI ZA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NA KUZUILIWA KWA MAWAKILI KUFANYA KAZI ZAO
UTANGULIZI
Mtandao wa Watetezi wa Waki za Binadamu (THRDC) kwa niaba ya wanachama wake zaidi ya 100 na kwa kushirikiana na Chama cha Wafugaji Tanzania, Baraza la Asasi za Kirai Tanzania NACONGO, Vyama vya Wanasheria vya Tanganyika na Zanzibar tunatoa tamko hili kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu, kushikiliwa kwa watetezi wa haki za binadamu/wafugaji kwa siku zaidi ya kumi bila dhamana, kunyimwa haki ya uwakilishi kwa watuhumiwa na mwisho kunyimwa kufanya kazi kwa wakili, kushikiliwa na kujumuishwa katika tuhuma za washitakiwa. Asasi za kiraia zinakemea matukio hayo kwa kuwa yanakiuka haki za binadamu na yanavunja Katiba ya nchi ya mwaka 1977.
Mtandao umepokea taarifa za kusikitisha za ukiukwaji wa haki za binadamu huko Loliondo hasa haki za watetezi wanaotambulika kuwa macho ya jamii ya wafugaji Loliondo. Mnamo tarehe 20 mwezi Julai, tulipokea taarifa za kukamatwa na kuwekwa kizuizini bila dhamana kwa watu saba akiwemo Mbunge wa zamani Methew Oletiman na madiwani wawili Mh Yanick Ndonyo, Ndina Timan, na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundoros Joshua Makko, Mkurugenzi wa Mtandao wa AZAKi Ngorongoro Samweli Nangiria, na wanaharakati wawili Supuk olemaoi na Clinton Kairung. Taarifa kutoka Loliondo zilisema wanashikiliwa kwa makosa ya kijasusi katika kituo cha polisi Loliondo kwa kuwasiliana na mwanahabari huru (mwanabloger toka) Sweden Susana Nurduland ambaye amekuwa mstari wa mbele kuandika taarifa za ukiukwaji wa haki za raia na migogoro ya ardhi Loliondo. Baada ya Mtandao kufuatilia kwa vyombo vya usalama akiwemo RPC Arusha, alisema timu inaendesha operation hiyo loliondo inaongozwa na Kamishna anayejulikana kwa jina Ryoba kutoka Makao Makuu Polisi Dar es Salaam. Kikosi hicho kilichopo Loliondo kimeundwa na maofisa toka taasisi mbalimbali zikiwepo TAKUKURU, UHAMIAJI, USALAMA, JESHI LA WANANCHI, POLISI nk.
Mnamo tarehe 21/07/2016, Mtandao kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) waliweza kutuma wakili Shilinde Ngalula pamoja na waandishi kufuatilia ukiukwaji huo na pia kuwapa uwakilishi wa kiwakili watetezi waliobaki ndani kwa takribani siku 9 sasa. Kilichotustua zaidi ni kuona siku ya tarehe 22/07/2016 wakili huyu kufukuzwa katika chumba alichokuwa akisimamia mahojiano ya watuhumiwa hao. Maofisa hao walionekana kumtishia wakili huku wakimweleza mahojiano hayo hayahitaji uwepo wa wakili na kuhoji nani kamtuma wakili huyo kuwasimiami watetezi hao wanataabika katika kituo cha polisi karibu siku tisa bila dhamana na bila kufikishwa hamahakamani.
Hatimaye siku hiyo hiyo jioni tarehe 22/07/2016 wakili Shilinde Ngalula alikamatwa na kujumuishwa na watuhimiwa huku akitamkiwa maneno kwamba na yeye alikuwa akitafutwa. Wakili alitoka kwa kujidhamini na kutakiwa kwenda Jumatatu tarehe 25 kwa kutoa maelezo yake kama watuhumiwa wengine. Kinachoshangaza, hadi sasa watetezi na wanaharakati wanane bado wameendelea kushikiliwa na kunyimwa dhamana huku watuhimiwa wengine wenye vyeo vya kisiasa wakipewa dhaman katika tuhuma hizo hizo. Watetezi wa haki za wafugaji loliondo wanaondelea kuwa chini ya ulinzi hadi sasa ni wanne Samweli Nangiria Mkurugenzi NGONET, Supuk Olemaoi, Clinton Kairung na Yohana Mako. Wamenyimwa dhamana, mahakamani hawapelekwi, wamenyimwa fursa ya kuonana na wanasheria na vifaa vyo vya mawasiliano vinashikiliwa zikiwemo komputa mpakato.
HALI YA WATETEZI NA MAWAKILI
Matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kukamatwa na kuhojiwa kwa watetezi wa haki za binadamu yamekuwa yakijitokezaa mara kwa mara huku kukiwa na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Serikali kwa Asasi za Kiraia ambazo zinatetea na kulinda haki za binadamu hasa swala la ardhi dhidi ya wawekezaji. Hivi karibuni tumeshudia baadhi ya watetezi kama Samweli Nangiria akifunguliwa mashitika, na viongozi wa serikali wakitoa maneno makali dhidi ya asasi za kiraia zilizopo Ngorongoro. Vitisho vimekuwa ni vingi na kupelekea watetezi na AZAKI kuanza kuhofia maisha yao na usalama wao. Wengi sasa wanaogopa kufanya kazi za utetezi na elimu kwa jamii kutokana na hali ilivyo sasa.
Vitisho hivi dhidi ya watetezi wa haki za raia, saa vinaonekana kuhamia hata kwa mawakili wanaojitolea kusimamia taratibu za kisheria kwa watumiwa. Tatizo hili lilianzia Zanzibar pale kiongozi wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipotoa tamko la kuwataka wanasheria waache kusimamia kesi za watuhumiwa. Kauli iliyotelewa Zanzibar na iliyotoka loliondo hazitofoutiana nah ii inatia hofu kubwa katika tasnia ya sheria kwani kazi za mawakili zipo kisheria na katika inatambua haki ya kuwakilishwa na wakili.
ANGALIZO
Wote kwa pamoja tunapenda kukumbusha serikali na vyombo vyake hasa Jeshi la Polisi kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 inataka vyombo vyote vya Serikali, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, kuhakikisha kwamba utu na haki nyinginezo za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa kwa mujibu wa ibara ya 9 (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Haki hizo ni pamoja na haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu ambayo inajumuisha haki ya kuwa na wakili, kwa mujibu wa ibara ya 13 (6) (a)
Ibara hiyo inasema hivi “ 13 (6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba–
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi na Mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya Mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika.”
Pia tunapenda kuwakumbusha Watanzana wote hasa, vyombo vya dola kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa za Mwaka 1990 za kazi za wanasheria zilizopitishwa mjini Havana, Cuba Tarehe 27 Agosti mpaka tarehe 7 Septemba 1990 ambapo Tanzania ni sehemu ya Umoja wa Mataifa zinatakamka yafuatayo:-
i. Kanuni ya kwanza inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kutetewa na Wakili wa chaguo lake kila hatua ya maamuzi juu ya shitaka lake.
ii. Kanuni ya 7 inazitaka Serikali kuhakikisha kuwa watu wanaokamatwa kwa tuhuma za makosa ya Jinai, ikiwa wamefikishwa Mahakamani au hawajafikishwa, wapate nafasi ya kuwakilishwa na Wakili katika muda usiozidi masaa 24 toka kukamatwa kwao. ( Huko Loliondo ni zaid sasa ya siku 8 watu wapo ndani).
iii. Kanuni ya 16 inazitaka serikali zote ikiwa, pamoja na serikali ya Tanzania, kuhakikisha Mawakili wanafanya shughuli zao bila vitisho, Manyanyaso au kuingiliwa kwa aina yoyote na chombo chochote.
Hivo kitendo cha kuwakamata wananchi kwa siku zaidi ya 8 bila dhama na muda huo kunyimwa haki ya uwakilishi basi vyombo hivo vinakiuka Katiba ya nchi, na wanaweza kushtakiwa muda wowote mahakani.
Lakini pia ifahamike kuwa mtu yeyote anayezuia au kutisha mawakili au wanasheria wasifanye kazi ya kuwatetea watuhumiwa wa Makosa ya Jinai, si tu kwamba anakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali mtu huyo pia anakuwa amekiuka sheria za nchi kwa sababu uwakili ni kazi ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na mawakili wamesajiliwa kwa mujibu wa sheria na kupewa leseni na Jaji Mkuu ama wa Tanzania ili wafanye kazi ya Uwakili.
Aidha, ikumbukwe watetezi wa haki za binadamu wakiwa mmoja mmoja au kupitia Asasi zao zilizosajiliwa kisheria wana haki ya kutetea raia na kutoa taarifa popote zinazohusu ukiukwaji wa haki za wananchi. Kitendo cha kuwanyanyasa watetezi wa haki za wafugaji loliondo kinakwenda kinyume na Azimio la Umoja wa Kimataifa la Watetezi wa haki Binadamu la mwaka 1998. Pia kwa kuwatishia na kuwakamata hovyo hovyo watetezi wa haki za raia na Asasi zao kunakiuka Katiba ya Tanzania inayolinda haki ya kujumuika.
WITO WETU
Kwa Asasi za kiraia
• Kuungana kukemea maswala haya ya uvunjifu wa haki za binadamu ambayo yamekuwa yakiendelea huko Loliondo an maneneo ya Tanzania kwa kipindi kirefu sasa.
• Kujumuika kwa pamoja na kuunda timu ambayo itasaidia kuchunguza na kushauri serikali jinsi ya kumaliza migogoro ya Loliondo iloyo dumu kwa muda mrefu sasa, huku ikiacha wananchi na watetezi wakiteseka.
Kwa Mahakama na Jaji Mkuu
• Tunamuomba Jaji mkuu pamoja na mahakama kuingilia swala hili la mawakili kukamatwa wakati wanatetea wateja wao
• Tunamuomba Jaji mkuu kutoa tamko kukemea vitendo hivi na ikidbidi kundwa tume huru ya kuchunguza swala hili la Lolilondo na kule Zanzibar la kuziiwa mawakili kufanya kazi zao na kuunganishwa na tuhuma za wateja wao.
• Wito pia kwa mawakili wote kuungana katika swala hili, na kuwaomba wasikate tama kuhakikisha haki za binadamu na misingi ya kisheria na Katiba ya nchi vinalindwa
Kwa wadau wa kimataifa
• Kuingilia kati swala hili na kukemea kwa pamoja
• Kuishauri serikali dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu ulio kisiri huko Loliondo
Kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vingne vya usalama
• Tunakumbusha Jeshi na vyombo vingne vya usalama kukumbuka kwamba nchi hii inaendeshwa kwa sheria na Katiba ya nchi, hivo kutumia sheria na sio madaraka yao binafsi.
• Tunawakumbusha Polisi na vyombo vya usalama kwa dhamana ni haki ya kikatiba na wakumbuke katika kutimiza majukumu yao kutambua kwamba mahakama pekee ndiyo yenye jukumu la kuhukumu.
• Tunatoa wito watumiwa wote waliodumu mahabusu kwa siku 5 hadi 8 sasa kinyume na sheria ,wapelekwe mahakamani tarehe 25/7/2015 kama wanamakosa au waachiliwe huru.
• Kwa kuwa mahojiano ya baadhi yao yalifanyika bila uwepo wa wakili tunatoa wito mahojiano ya watuhumiwa hao yarudiwe na kufanyika mbele ya wakili.
IMETOLEWA LEO TAREHE 24/7/ 2016
WANACHAMA THRDC
1 ASSOCIATION FOR NON- GOVERNMENTAL ORGANIZATION ZANZIBAR [ ANGOZA]
2 BETHANIA EMPLOYMENT AND SUPPORT [ BEST]
3 BETTER LIFE [ NGO]
4 BIHARAMULO NON- GOVERNMENTAL ORGANIZATION NETWORK [ BINGO FORUM}
5 CESOPE
6 DUNGONET [Ngo’s Network for Dodoma Urban}
7 HAKI MADINI
8 HAKI ZA BINADAMU NA ZA RAIA
9 JUKWAA LA KATIBA
10 KASULU LEGAL AID
11 KIGOMA WOMAN DEVELOPMENT {KIWODE}
12 LEWOPAC
13 LHRC
14 MBEPAU
15 MBEYA hope for orphans
16 MBEYA WOMAN
17 MISA TAN
18 MKEMBA GROUP
19 MOIPAC
20 MTWARA PARA LEGAL
21 MUSODEO
22 PAICODEO
23 LESHABINGO
24 PARALEGAL PRIMARY JUSTICE
25 PINGOS FORUM
26 RURAL WOMAN DEVELOPMENT INITIATIVES [RUWODI}
27 RUVUMA PRESS CLUB
28 SAHARINGON
29 SERVICE HEALTH AND DEVELOPMENT FOR PEOPLE
30 SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU NANDANGALA
31 SIKIKA
32 TAMWA
33 TANZANIA LEGAL KNOWLEDGE AID CENTER {TALAKACE}
34 TANZANIA NETWORK OF LEGAL PROVIDERS {TANLAP}
35 TANZANIA PARTNERSHIP DEVELOPMENT ORGANIZATION
36 TANZANIA PASTORALIST COMMUNITY FORUM {TPCF}
37 TANZNIA PEACE,LEGAL AID AND
38 TANZANIA YOUTH POTENTIAL ASSOCIATION
39 TAS
40 TAWLA
41 TCIB
42 TGNP MTANDAO
43 THE ORGANIZATION OF JOURNALISTS AGAINST DRUG ABUSE AND CRIME IN TANZANIA { OJADACT} AJAT
44 TUPACE
45 UNDER THE SAME SUN
46 UTPC
47 WORLD YOUTH ALLIANCE
48 YOUTH TO YOUTH
49 ZAFELA
50 ZANZIBAR AIDS ASSOCIATION AND SUPPORT OF ORPHANS ORGANIZATION [ZASO]
51 ZANZIBAR ASSOCIATION FOR CHILDREN ADVANCEMENT [ZAC]
52 ZLSC
53 TANZANIA WIDOWS ASSOCIATION
54 RUANGWA ORGANIZATION FOR POVERTY ALLAEVIATION [ROPA]
55 TANZNIA PEACE LEGAL AID AND JUSTICCE CENTRE
56 DEFENCE OF HUMAN RIGHT /CITIZEN RIGHT [DHR/CR]
57 NGUVUMALI COMMUNITY DEVELOPMENT OF ENVIRONMENT
58 TANZANIA LEGAL KNOWLEDGE AND AID CENTRE
59 MBEYA HOPE FOR ORPHANS [MBEHO]
60 SHDEPHA - BIHARAMULO
61 RESOURCES ADVOCACY INITIATIVE [RAI]
62 MUKEMBA GROUP MAENDELEO
63 PARALEGAL PRIMARY JUSTICE [PPJ]
64 BIHARAMULO NGOS NETWORK FORUM
65 THE DEVELOPMENT FOR ACCOUNTABILITY FOR TANZANIA
66 HUMAN RIGHT NATIONAL ASSOCIATION OF EDUCATORS FOR WORLD PEACE
67 MTWARA PARALEGAL CENTRE
68 MIKONO YETU CENTER FOR CREATIVITY AND INNOVATION {[MIKONO YETU]
69 MEDIA ASSOCIATION FOR INDIGENOUS AND PASTORALIST COMMUNICATIES
70 GOSPAL COMMUNICATION NETWORK OF TANZANIA
71 TANZANIA MEDIA WOMAN’S ASSOCIATION
72 RURAL WOMAN DEVELOPMENT INITIATIVE [RUWODI
73 WOTESAWA YOUTH DOMESTIC WORKERS
74 Tanzania Centre for Research and Information on Pastoralism
No comments:
Post a Comment