Sunday, 24 July 2016

MOYES APATA KIBARUA SUNDERLAND

OFFICIAL: SUNDERLAND WAMTHIBITISHA MOYES KUA KOCHA MPYA.



Kocha wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester united na Real Sociedad ametangazwa rasmi kua kocha mkuu wa paka weusi (klabu ya soka ya Sunderland) kuchukua mikoba iliyoachwa na Sam Allardeyce ambaye analwenda kuifundisha timu ya taifa ya England (Simba watatu).


Moyes amesaini mkataba wa miaka minne ya kufanyakazi katika uwanja wa stadium of Light. Inakua ni mara yake ya kwanza kurejea kufanya kazi EPL tangu alipotimuliwa na Manchester united April 2014. Mwenyekiti wa Sunderland alisema wanafurahia kumkaribisha David Moyes kwenye klabu ya Sunderland kwani yeye alikua ndiye chaguo la kwanza la klanu hiyo. Aliongeza pia kua ukweli kua David Moyes amesaini mkataba wa miaka minne ni uthibitisho tosha wa imani yake kwa kile ambacho anaweza kukipata akiwa hapa.

Kwa upande wake David Moyes hakusita kuelezea furaha yake ya kupata nafasi ya kufanya kazi tena kwenye EPL kwa mara nyingine tena.

No comments:

Post a Comment